Friday, November 27, 2015

VITUKO TANZANIA NA VICHEKESHO;WEWE HUFANYI LIPI KATI YA MAMBO HAYA KUMI (10) YA KUCHEKESHA NA KUSHANGAZA


1. Kukaa peke yako na kuanza kupiga hesabu kwa pesa ambayo hauna, utakuta kijana ametulia anaanza kupiga mahesabu nikipata milioni 10 nitafanya 1, 2, 3,……n.k. Na hii huwatokea vijana wengi sana.
2. Kupiga piga rimoti na kubonyeza wakati tunajua kuwa betri zimeisha na ikikubali hununui tena betri utazani tatizo limeisha kumbe lipo pale pale.
3. Kutoboa tube ya dawa ya meno au kopo la mafuta ili kukombeleza masalia kwa ajili ya kutumia.
4. Kusimama mbele ya kioo na kuanza kujitizama huku ukiweka mapozi mbalimbali kwa maringo. Unashtuka kuna mtu alikuwa anakuona unaanza kuzuga.
5. Kufanya usafi siku anapokuja mgeni, na hii iko hasa kwa vijana wanaoishi “getto” na pia wadada wengi huwa na nguo za ndani zilizotoboka wakidai ni za kuvaa nyumbani, sijui siku ikitokea dharura itakuwaje mi simo.
6. Kuongea na simu huku ukifanya mambo mbali mbali ya ajabu unaweza ukapewa hata moto na ukapokea au kuweka kiatu ndani ya friji yaani akili yako inakuwa haiko eneo husika kabisa.
7. Unasoma kitabu au kitu chochote lakini akili yako haipo na unakuja kushtuka uko kurasa ya tatu au ya mbele zaidi na hujaelewa chochote. Hahaah.
8. Upo katikati ya watu mara simu inaita unaangalia kama ni simu yako wakati mlio wako haufanani kabisa na mlio ulioita. Hahaah...
9. Umeongozana na mtu mnapiga stori ghafla anasimama wewe hujui unaendelea tu kuongeana mtu mwingine wala hata hakufahamu unakuja kushtuka mbali sana. Dah aibu
10. Umekutana na mtu unahisi kama unamfahamu na unaanza kumuuliza kasoma wapi ili ujuemlikutana mazingira gani masikini kumbe ulimuona kwenye TV.

Author:

0 comments: