Ni kutoka katika Jitambue Sasa.
Unaweza ukaziita Ni KANUNI AU SHERIA AU LAWS.
Akili ya mwanadamu ni sehemu ambayo watafiti wengi wamekuwa wakihamasika kuielewa. Akili ni sehemu pana sana kwa mwanadamu. Ni sehemu ambayo haionekani wala haishikiki lakini ina matokeo makubwa sana kwa mwanadamu. Akili imezaa vitu vilivyotengenezwa na mwanadamu, mawazo, imani, misimamo n.k. Kama unapenda sana kujifunza na kufahamu mengi lazima utakuwa unatamani kufahamu siri kuu za akili. Kuelewa siri kuu za akili ni kufahamu Sheria ambazo zinaiongoza akili. Katika mada hii utapata kuona mwanga kuhusiana na akili na kuweza kujifahamu vyema.
SHERIA/KANUNI HIZO NI:
- Sheria ya Chanzo na Matokeo
- Sheria ya Uhuru wa Kufikiria
- Sheria ya Umakini/focus
- Sheria ya Mawazo
- Sheria ya Ubinafsi
- Sheria ya Uumbaji
- Sheria ya Hisia
- Sheria ya Ubadili
- Sheria ya Usawa wa Akili
- Sheria ya Kutokea.Nini maana ya Sheria za Akili?
Mapinduzi makuu ya sasa ni ufuatiliaji wa asili na jinsi akili ya mwanadamu ilivyo. Sayansi ya kufuatilia akili ya mwanadamu ilivyo ni sayansi ambayo inategemewa kuleta mapinduzi makubwa kwani akili ya mwanadamu ina sayansi kubwa sana. Asilimia kubwa ya maisha ya mwanadamu inatengenezwa na akili yake hivyo katika elimu hiyo utaweza kufahamu mengi sana kuhusiana na mwanadamu na jinsi akili yake inavyofanya kazi vyema.
Mlolongo huu wa mada utakuwa na mada kumi, ambapo kila mada itaelezea sheria yake kwa undani kwani kuweka mada moja kuelekeza mad azote hizi kutapelekea uchache wa maelekezo.
Sheria
Kwa lugha nyingine huita “Laws”. Sheria ni kama maelekezo ya suala au jambo Fulani. Wengi wanafahamu sheria ya mvutano, ni sheria inayosema kuwa ukirusha kitu juu basi huvutwa kwenda chini kuelekea ardhini. Ni sheria ambayo uwe unaijua au usiijue ukijirusha gorofani lazima uanguke chini. Sheria kuwepo haimaanishi mpaka uijue ndipo matokeo yake huonekana bali hata ukiwa haujui bado sheria itafanya kazi yake katika mangilio wake unavyotaka.
Zipo sheria mbalimbali ulimwenguni ambazo zimekuwa zikilinda taratibu nyingi. Je umewahi kujiuliza kama kuna sheria au taratibu Fulani ambazo ukizielewa utaweza kufahamu jinsi akili inavyofanya kazi? Ni sawa na mkulima, akipanda maembe atavuna maembe, hata kama anajua kuwa anavuna anachopanda au hajui kuhusiana na uhusiano uliopo kati ya anachovuna na anachopanda bado atapata matokeo sawa. Hivyo ni vyema kufahamu sheria hizo. Ni vyema kufahamu kwani itakusaidia kuweza kuongoza matokeo. Ukiwa unajua kuwa taratibu Fulani hupelekea matokeo Fulani inakusaidia kutengeneza wakati ujao katika njia njema na kupata matokeo mazuri.
Mfano wa sheria nyingine ni sheria za rangi, kila mmoja anafahamu ukichanganya nyekundu na njano unapata machungwa, ni sheria kwani lazima itokee hivyo. Uwe unajua hilo wakati unachanganya au haujui lakini lazima matokeo yake yatokee. Ukichanganya blu na yellow utapata kijani, hiyo ni lazima. Labda uwe haujachanganya vyema au tatizo linguine lakini zikishachanganyika matokeo yake ni mengine.
Lengo la kutoa mifano hiyo ni kukupa mwangaza wa kuwa kuna sheria hapa ulimwenguni. Sheria ni taratibu ambazo zipo. Taratibu hizo hupelekea matokeo Fulani katika taratibu Fulani. Ni vyema kufahamu taratibu za msingi kuelewa mengi kwani ulimwengu upo kwa taratibu maalum. Kama tungekuwa hatujui kuwa ukiruka gorofani utaanguka chini na kufa kwani ukiruka unaanguka chini ni wangapi wangekuwa wamekufa kwa kutojua hayo? Lakini anayeuuzia hayo au kufanya maamuzi bila kujali au kwa kujali lazima taratibu zichukue nafasi yake na kupelekea matokeo yake.Kama dunia ilivyo na sheria zake, serikali zilivyo na sheria zake, dini zilivyo na sheria zake, tamaduni Fulani za watu zilivyo na sheria zako fahamu kuwa hata akili nayo ina sheria zake. Kuna sheria za biolojia, jeographia, fizikia, n ahata saikolojia. Fahamu kuwa na hata akili ina sheria zake. Sheria hizo hutawala maisha ya mwanadamu kwani kila mwanadamu ana akili yake lakini akili zote zina asili moja na sheria moja, tofauti ni utumiaji.Sheria zilikwepo tangu mwanzo wa ulimwengu na zitazidi kuwepo. Huenda kuna sheria nyingi ambazo bado hatujazijua kutokana na uelewa wetu lakini haimaanishi hazipo, bado zipo tu. Galileo Galilei alipofahamu kuwa kuna Gravity na kuelezea sheria ya kuvutwa vitu chini haimaanishi kabla yay eye kuelezea ilikuwa haipo. Bali alichofanya yeye ni kuifahamu sheria na sio kuianzisha sheria. Unaweza ukatumia sheria kwa mafanikio. Mfano kutokana na uelewa kuwa kuna kani ya mvutano wa tumetengeneza meli (kwa kuhakikisha haizami), tumetengeneza ndoo na vyomba vya kuhifadhi maji kwa kuziba chini, n.k vyote hivi ni kutusaidia kuweza kuishi katika cheria tulizozikuta.
Fahamu kuwa unaweza kuiongoza akili yako na kuitawala akili yako. Akili ni chombo kizuri sana kwa kubadilika lakini pia ni chombo kibaya sana kwa kupotoka.
Mada za Kuhusiana na Sheria hizo zinafuta, na kila sheria itaelezewa katika mada yake na mifano hai ambayo itakufunua mwangaza na kuelewa vyema jinsi akili ya mwanadamu ilivyo ya ajabu.
Mawazo yetu ndiyo yanayounda uhalisia wetu na sio vingine. Hii ni sheria ya kale sana tangu enzi za wanadamu wa kale waliopenda kuwa watafutaji wa ukweli wa ulimwengu walikutana nayo. Ni sheria ambayo inafahamika sana na imetafsiriwa katika maelezo tofauti tofauti katika imani tofauti tofauti.
Ni sheria Kuu.
Kama ilivyo leo, hakuna anayefahamu ni kwanini kuna sheria kama vile ya Gravity, sheria za sayansi, n.k. Na hata katika sheria hii hakuna anauejua kwanini sheria hii ipo lakini hiyo haijalishi, kinachopaswa kwetu sisi wanadamu ni kuielewa vyema na kujua jinsi inavyofanya kazi ili nasi tuweze kuishi nayo.
Wazo ndio chanzo, vingine vyote ni matokeo tu.
Watu wengi hasa ambao hawajasoma sana wanafikiri kuwa vitu vya kifizikia ni halisi, wanafikiri ni kweli vitu hivyo vipo kifizikia. Kutokana na uelewa wao huo wanakuwa wanaamini sana ulimwengu wa nje yao na kusahau ulimwengu wa ndani yao. Huwezi kuelewa ulimwengu wa nje bila kuelewa ulimwengu wa ndani, ulimwengu wa nje ni matokeo ya ulimwengu wa ndani. Kutokana na kutoelewa huko watu wamekuwa wakiteseka na kuamini hawawezi kubadili maisha yao kwani hawajui chanzo cha maisha yao. Hawafahamu kuwa maisha yako ni matokeo ya uelewa wako wa ndani yako.
Mfano mzuri katika kuelewesha hilo ni sawa na tunaangalia sinema, kumbe sinema hiyo inatokana na matukio yaliyopo ndani ya ufahamu wetu. Sio sinema iliyopo nje yetu bali chanzo chake cha matukio kinatokana na ufahamu wetu. Sinema yake ni kama display tu ya ufahamu wetu. Kutoelewa hayo wanadamu wengi wamekuwa watumwa na wanateseka kutokana na kutofahamu chanzo cha hayo yote ni nini.
Kumbuka kuwa tunapoangalia sheria za kifizikia tunafahamu dhahiri kuwa HAKUNA JAMBO LISILO NA CHANZO. Na sheria hii ndipo iliposimamia. Hakuna jambo lisilo na chanzo na ndio maana inaitwa sheria ya chanzo na matokeo kwani kila tokeo lina chanzo chake. Hakuna matokeo yasiyo na chanzo kamwe.
Hivyo kama kila jambo lina chanzo chake, tunapaswa kufahamu kuwa uhalisia/reality ni illusion/Uongo kwani reality inatengenezwa na sisi wanadamu wenyewe na sio kwingine. Reality au uhalisia unaoishi unatokana na milango yako ya ufahamu, akili yako, imani yako na uelewa wako.
Kila kitu kina chanzo, huo ni uhalisia. Kila kitu kilianza kama ufahamu, mfano mzuri ni Computer, madirisha, nyumba, simu, nguo, sanaa, na vyote ambavyo vimetokana na ujuzi wa mwanadamu vilianza kama WAZO, baada ya kufanyiwa kazi vikatokea katika dunia ya kifizikia. Lakini hapo kabla vilikuwa ni Mawazo na sio physical things.
Chunguza sana sheria hii, kila tokeo unaloliona lina chanzo chake, kufahamu sheria hii inakusaidia kuwa mtafutaji wa ukweli. Badala ya kupoteza nguvu katika matokeo unapaswa kufuatilia chanzo cha tokeo kwani kubadili chanzo ni kubadili matokeo.
Walimu wakubwa wa ulimwengu huu wote wamefundisha sheria hii, wanaweza wakawa hawajakuambia moja kwa moja kutokana na kuwa uelewa wa wanadamu unatofautiana kwa jinsi wanavyoutumia lakini walimu hao wamekuwa wakitufundisha vyema kwa mifano. Mfano mzuri ni kuwa
- Unavuna unachopanda: Ukipanda maembe utalima maembe, ukipanda magugu utavuna magugu. Sheria hii ni sawa na kukuambia kuwa kila tokeo lina chanzo, kubadili chanzo ni kubadili matokeo. Huwezi kuvuna maembe katika tawi la mchungwa.
- Sheria ya Karma: Ni sheria ya mashariki inayosema kuwa kila WAZO, TENDO na MANENO yana matokeo yake katika ulimwengu wako. Kutokana na hilo wakafundisha kuwa kuna Karma ya matendo, Kuna karma ya maneno na kuna karma ya mawazo. Hivyo kila tutendacho, tusemacho na tunachofikiria kina matokeo katika dunia yetu. Nimesema dunia yetu kwani kila mwanadamu anaishi katika dunia yake. Sheria hii nayo nitakuja kuieleza vyema.
- What goes around comes around: Nayo ni sawa na kusema kuwa kunachokijia ni matokeo ya kilichotoka kwako. What comes around is the result of whats goes out of you. Unachokipata ni matokeo ya ulichokitoa.
Tutakapokuja kufahamu kuwa tunaishi katika ulimwengu unaoumbwa kutokana na ufahamu wetu, kwa kufahamu hayo ni hatua moja ya kwanza katika kuweza kubadili maisha yako na kuweza kuelewa kwanini wanadamu wengine nao wanaishi katika uhalisia tofauti na wewe. Kwa kuanza kuelewa hili utaweza kujiuliza mengi na kujikuta unafahamu chanzo cha mengi badala ya kupoteza muda katika matokeo. Wengi hupoteza muda kubadili matokeo kumbe matokeo ni matokeo, huwezi kuyabadili bali unaweza kubadili chanzo chake.
Maya Angelou aliwahi kusema sentensi moja nzuri sana -Kama haupendi unachokiona kibadili, kama hauwezi kukibadili badili mtazamo wako.
Kwa kuweka sheria hii katika uelewa mzuri na kwa kufupisha vyema ni kusema kuwa:
Mawazo yetu yanaumba ulimwengu wetu, mawazo yetu ndio kiaishiria ya kinachofuatia. Kila jambo lina chanzo, chanzo kikuu na chanzo ambacho ndio cha mwanzo kabisa ni WAZO. Tunaishi katika dunia ambayo inatengenezwa na uelewa wetu. Ndio maana kila mwanadamu anaishi katika dunia yake kutokana na kuwa uelewa unatofautiana baina ya wanadamu.BADILI MAWAZO YAKO KUBADILI DUNIA YAKO.Sheria Kuu Kumi za Ulimwengu na Akili (10 Laws of the Mind and Universe/Universal LawsNi kutoka katika mada ya kwanza iliyokuwa inaelekeza umuhimu wa akili, mawazo na imani katika kuumba uhalisia wa maisha yetu. Baada ya kuelewa kuwa kuna uhusiano kati ya Akili na Wazo katika maisha yetu sheria hii ya pili kuielewa sio taabu kwani kila mmoja anafahamu hivyo.
Sheria ya Uhuru wa Kufikiria.
Sheria hii inasema kuwa "wewe pekee ndiye unayefikiria katika akili yako". Sheria hii inamaana kuwa hakuna mwanadamu yoyote, being yoyote, wala kwa wanaoamini malaika na majini na chochote, vyote hivyo hakuna anayefikiria kwa kutumia akili yako bali wewe mwenyewe ndio Thinker/Mfikiriaji.
Hakuna anaweza kutumia akili yako kufikiria, kila mtu ana akili yake, wakati huo huo wote tunaunganishwa na Mind kuu moja, Mind hiyo wengi wanaiita kitofauti tofauti kutokana na uhalisia wao na uelewa wao. Kila mmoja ana uhuru wa kufikiria. Kila mmoja ana uhuru wa kutumia akili yako kivyovyote.Kuelewa ufahamu huu ni faida kubwa kwani utaelewa kuwa kila mtu anatumia akili yake kivyake. Hakuna anayeweza kufikiria katika akili yako bali wewe mwenyewe. Una uwezo wa kuwaza, kuamini, kufikiria na kuelewa vyovyote, ni wewe mwenye maamuzi. Huo ni uhuru wa mwanadamu.
Hakuna mnyama anayeweza kuwaza anachotaka, wanyama huongozwa na hisia, hormones, insticts n.k lakini hawawezi kufanya uhuru wa maamuzi ulio nao wewe mwanadamu. Ni maajabu makubwa na ni baraka. Japokuwa hakuna anayejua ni kwanini hivyo, hakuna anayejua ni kwanini kazaliwa mawanadamu, bali tunachojua ni kuwa sisi ni wanadamu na tuna upekee mkuu sana katika utajiri tulionao na uwezo wetu wa kuyaelewa maisha kiundani zaidi ya aina nyingine zote za maisha. Nimesema aina zote za maisha kumaanisha mimea, wanyama, wadudu n.k kwani wote hao pia wana uhali, lakini hawana uhuru wa kutumia akili yao watakavyo.
Baada ya kuelewa ufahamu huu, utajikuta hausemi kuwa "ninafikra fulani kwa sababu nimefundishwa hivyo", au mwingine kuamini kitu fulani kwa sababu wazazi wamemfundisha, au marafiki, vikundi cya watu, na kadhalika. Wewe ndiye mwenye maamuzi, hakuna anayeweza kufikiria katika akili yako zaidi yako wewe mwenyewe.
Watu au hali zinaweza kukuhamasisha tu lakini haziwezi kukufanyia maamuzi. Hata katika imani zinazoamini Kuwa kuna shetani, hazifundishi kuwa shetani anaweza kukufanyia maamuzi bali wewe mwenyewe ndio muamuzi.
Kitu chochote unaweza kukitumia katika usahihi au katika ubaya, hata akili ya mwanadamu inaweza kutumika katika usahihi au katika ubaya.
Kwa kuhitimisha ni kuwa, sheria hii inatusaidia kufahamu kuwa wewe ndiye mwenye maamuzi makuu katika utumiaji wa ufahamu wako. Utakavyotumia ufahamu wako ndivyo uhalisia wako utakavyokwepo. Ufahamu wako unaumba dunia/ulimwengu wako hivyo ni vyema kutumia uhuru huu kutengeneza uhalisia wako uupendao.
Una uwezo wa kuamua unachotaka kufikiria. Kama unaona unafikiria mawazo mabaya sana, wasiwasi, matatizo, shida, unaweza kubadili mtazamo wako na kuwaza ya muhimu na kushukuru kwa kila hali badala ya kuumia na hali. Haijalishi mambo yanayokuzunguka ni magumu kiasi gani, haijalishi una mawazo kiasi gani, kinachojalisha ni kuwa una uhuru wa kuwaza na kuelekeza fikra yako unapopenda na fahamu kuwa popote utakapoelekeza fikra zako panakua na kufanyika uumbaji.
Kujizoesha kuweka fikra ni kama aina nyingine za ujuzi, kama unavyoweza kujifunza kusoma, kuandika, n.k pia hata kujua kuongoza ufahamu na fikra yako ni mazoea tu. Ni kujizoesha kuwaza fikra fulani na mwishowe fikra hiyo inakukaa na unaweza kutumia uhuru wako utakavyo.Akili ni kama farasi pori, ni vigumu kumuelewa lakini ukiweza kujenga urafiki naye na kumuongoza, ana nguvu kubwa katika kukusaidia lakini ukishindwa kumuongoza atakuendesha bila wewe kujijua.
| 1:38 PM
0 comments: