Monday, November 30, 2015

LEE MIN HO,MKALI WA CITY HUNTER ANAYE MUHUSUDU RONALDO

                                                              

Anajua kupendeza,ana pesa na amesoma,anapiga huyoo ni hatari sana.Alizaliwa mji mkuu wa korea kusini,seoul mwaka 1987 june 22.Anaitwa LEE MIN HO,mkali wa tamthilia ya CITY HUNTER na BOYS OVER FLOWER.

Akiwa mdogo,ndoto yake ilikuwa kuwa mcheza mpira maarufu.Alichaguliwa kujiunga na kituo cha vijana cha mpira wa miguu nchini korea kusini lakini ndoto zake zilipotea baada ya kuvunjika mguu akiwa daraja la tano la elimu ya awali.Kwake mchezaji bora wa zama hizi ni CHRISTIAN RONALDO wa Real Madrid,anamkubali sana na anaamini kama asingeumia basi angekuwa kama yeye.Alianza kuigiza akiwa mwaka wa pili wa high school.
Mwaka 2006 alipata ajari mbaya ya gari iliyomlaza wodini kwa muda mrefu.

Miaka ya mafanikio(2009-2012)

Mwaka 2009 alicheza tamthlia ya BOYS OVER FLOWERS ambayo ilifanya vizuri sokoni na kumletea umaarufu mkubwa sana.Alichaguliwa kama muigizaji bora mpya ma mwaka huo.2011 ndiyo ilikuwa hatari kabisa baada ya CITY HUNTER kuingia sokoni.Ni bonge la tamthilia na iliyomletea mafanikio sana.Alichukua tuzo Zaidi ya nne na mafanikio makubwa ya kiuchumi.Mwaka 2012 aliachia kitu kingine kikali,FAITH tamthilia ya kihistoria ya kutumia,ameonyesha utaalam mkubwa wa kutumia mapanga ya kivita.
Mwaka 2011 pia alilipotiwa kuwa na uhusiano na muigizaji mwenzio wa CITY HUNTER,KIM NANA ingawa waliachana mwaka 2012.
Mwaka 2014 alikuwa muigizaji wa kwanza kutoka korea kusini kuhudhulia kipindi cha kichina kiitwacho CCTV LUNARNEW YEAR GALA ambacho huangaliwa na Zaidi ya wachina milioni 800 duniani kote.Sasa hivi yupo katika uandaaji wa tamthilia iitwayo BOUNTY HUNTERS.


Tukutane kwenye post nyingine ya tamthilia za kikorea,kwa maoni na mapendekezo ya nani tumuandike,tuma kwenye sanduku la maoni hapo chini.

Author:

0 comments: