Sunday, January 24, 2016

Kilichomponza Dk. Mwaka Chafichuka..Nimekuwekea Hapa A to Z

Kilichomponza Dk. Mwaka Chafichuka..Nimekuwekea Hapa A to Z


Stori: Deogratius Mongela na Chande Abdallah

SIRI nje! Sakata la mmiliki wa Kliniki ya Tiba Asilia ya Fore Plan iliyopo Ilala Bungoni, Dar, Dk. Juma Mwaka ‘JJ Mwaka’ kufanyiwa ziara ya kushtukiza na baadaye kudaiwa kumkimbia Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Hamis Kigwangalla limechukua sura mpya huku mambo mengi yaliyomponza yakifichuka, Risasi Jumamosi limechimba.
Dk. Kigwangalla akiingia kwenye Kliniki ya Tiba Asilia ya Fore Plan.
SOO LILIVYOKUWA
Siku chache baada ya kuteuliwa kuwa naibu waziri, Dk. Kigwangalla alifanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho kinachosifika kwa kutoa tiba ya asili badala ya hospitali (tiba mbadala), hasa kwa wanawake wanaosumbuliwa na matatizo ya uzazi.
Katika hali ya kushangaza, matatibu na manesi waliokuwa kazini walitokomea kusikojulikana na kuwatelekeza wagonjwa, wakikwepa kuonana na waziri huyo ambaye akiwa na msafara wake, walifanya ukaguzi wa kina kwenye kituo hicho.
Kufuatia kitendo cha Dk. Mwaka na wenzake kuingia mitini, Waziri Kigwangalla alitoa amri ya kufungwa kwa muda kwa kituo hicho mpaka uchunguzi wa kina utakapokamilika ili kuona kama huduma zinazotolewa zinakidhi vigezo na ni salama kwa wagonjwa.
Nyumba ya Dokta Mwaka JJ 
MITANDAO YAMCHOMA
Simulizi ya jinsi tabibu huyo alivyosimamishwa kutoa huduma ili kupisha uchunguzi na ukaguzi wa kina, inaanzia mbali ambapo kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya kuaminika, chokochoko kuhusu huduma zake zilianzia kwenye mitandao ya kijamii.
“Kwa kipindi kirefu kulikuwa na makundi mawili yanayoshindana kwenye mitandao ya kijamii. Kundi la kwanza ni wale waliowahi kutibiwa katika kliniki hiyo na kufanikiwa kupona matatizo yao.
“Hawa walikuwa wakimtetea kwamba anatoa huduma sahihi lakini kundi jingine ni wale waliotibiwa na kupoteza fedha nyingi bila kupona matatizo yaliyokuwa yakiwasumbua.

“Hawa ndiyo waliochangia kwa kiasi kikubwa kuifumbua macho Serikali ya Rais John Pombe Magufuli kwani walitaka dawa na huduma za Dk. Mwaka zichunguzwe kwa vile walishapoteza imani naye,” kilisema chanzo chetu makini kwa sharti la kutoandikwa jina gazetini.
Gari lake, ania ya Range Rover-Sport SE
KUANIKA MAISHA YAKE MTANDAONI
Kwa mujibu wa chanzo kingine, tabia ya Dk. Mwaka kupenda kuanika maisha yake kwenye mitandao ya kijamii ni suala jingine lililomponza na kufanya watu waanze kutilia shaka utajiri wake.
“Unajua Dk. Mwaka na mkewe wamekuwa wakiposti kwenye mitandao ya kijamii, hasa Instagram picha za magari yao ya kifahari anayomiliki likiwemo Range Rover-Sport SE na hekalu (jumba kubwa la ghorofa) analoishi, lipo Mbezi (Dar).
“Pia walikuwa na kawaida ya kujisifia wanaposafiri kwenda nje ya nchi kufanya shopping, hasa Dubai. Hicho pia kimemponza sana maana watu walianza kufuatilia utajiri wao na pengine ndiyo waliomchongea serikalini,” kilisema chanzo hicho kilicho karibu na familia hiyo.
VIPINDI RUNINGANI

Sababu nyingine inayotajwa na vyanzo vyetu kwamba imemponza tabibu huyo, ni ile kawaida yake ya kuendesha vipindi kwenye runinga, akieleza huduma anazozitoa kwa lengo la kupata wateja wengi.
“Unajua Dokta Mwaka ndiye anayeongoza kwa kuwa na vipindi vingi vya runinga kwenye televisheni mbalimbali nchini. Kama unavyojua kipindi kimoja cha runinga kulipia kinagharimu fedha nyingi sana. Sasa watu wakawa wanajiuliza anapata wapi fedha za kulipia gharama hizo? Ni kutoka kwa wateja wake kweli?” kilisema chanzo chetu.
KUPUUZA AGIZO LA WIZARA

Pia, habari za ndani zinadai kuwa, mwaka jana wizara husika iliwaita wataalam wote wanaotoa tiba mbadala na kuwapa masharti.
Masharti hayo ni kutovaa koti jeupe, kutoning’iniza shingoni chombo cha kusikilizia mapafu/mapigo ya moyo (stethoscope) na kutojiita madaktari wakitakiwa kutumia utambulisho wa tabibu masharti ambayo karibu wote wameyapuuza.
KUNA KOSA KUJITANGAZA?

Katika utafiti uliofanywa na gazeti hili na kutiliwa nguvu na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu imebainika kwamba, kwa mujibu wa viapo wanavyokula madaktari na matabibu ni makosa kujitangaza kwenye redio, runinga au mitandao kwa lengo la kuwavuta wagonjwa.
“Changamoto iliyopo kwetu ni kwamba matangazo wanayoyatoa ni kinyume na kanuni lakini tumebaini kwamba Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambayo inasimamia sekta ya mawasiliano na utangazaji nchini ndiyo inayoruhusu. Tumejipanga kukutana nao ili kujadili jambo hili,” alisema Mwalimu.
SIYO MARA YA KWANZA KUFUNGIWA
Tukio hili la kusimamishwa kutoa huduma, si la kwanza kumtokea Dk. Mwaka ambapo mwaka jana, maafisa kutoka wizara ya afya walifika kwenye kliniki hiyo kwa kushtukiza, wakiwa wameongozana na waandishi wa habari na kufanya ukaguzi ambapo kutokana na kutoridhishwa na mazingira waliyoyakuta, walilazimika kuifunga kliniki hiyo kwa muda usiojulikana.
Hata hivyo, wiki kadhaa baadaye, Dk. Mwaka alifungua kesi mahakamani kupinga kufungiwa huko na kushinda kesi.

Sakata la Katibu wa Yanga Kuondoka Yanga..Manji Afunguka Mazito

TAARIFA KWA WANAYANGA KUPITIA VYOMBO YA HABARI
1. Baada ya kuupitia uamuzi wa Kamati ya Nidhamu kuamua sababu kuvunja mkataba kati ya klabu Yanga na mchezaji Haruna Niyonzima, nilihisi kulikuwa kuna kasoro hasa kwa mchezaji anayelipwa mshahara wa Sh milioni 6 anaweza vipi kupuuzia maisha yake na kuanzisha mgogoro usiokuwa na tija kwa maisha ya kipato. (angalia kiambatanisho 1)

Niliamua uchunguzi wa ndani ufanyike katika suala hilo zima na mwisho, Jonas Tiboroha alibainika kuwa hakuwasilisha ushahidi ya mawasiliano sahihi kwa Kamati ya Nidhamu kuhusiana na Haruna Niyonzima, hali iliyosababisha kamati kuchukua uamuzi ambao haukuwa sahihi kwa sababu;
Kulifanyika mambo ambayo hayakuwa sahihi, mfano barua za Niyonzima kutoka kwa Shirikisho la Soka la Rwanda (Ferwafa) ambazo zilitumwa kwa TFF na kupokelewa kama ambavyo Azam FC walipokea ya mchezaji wao kupitia kwa Afisa Mtendaji Mkuu wao. Lakini barua ya Niyonzima kuja Yanga, ilionekana haikupokelewa kama ilivyokuwa kwa barua yake ya utetezi na ile ya kuomba radhi alizoandika, nazo zilipokelewa lakini hazikuwasilishwa kwenye kamati ya nidhanmu na hili, mhusika ni Tiboroha.

kiachana na kamati kufanya uamuzi usio sahihi, hili pia limemjengea mchezaji chuki kubwa kwa wanachama na mashabiki. (angalia kiambatanisho 2 & kiambatanisho 3)

Kamati ya Utendaji (EXCOM), bada ya kupitia kwa kina iliona uamuzi ilichukua haukuwa haukuwa ya haki kutokana na kupotoshwa na Tiboroha tena aliendelea kuipotosha kamati kwa makusudi kutokana na kuficha nyaraka hizo ili Niyonzima afukuzwe. Tulifikia maamuzi Tiboroha alikuwa na ajenda yake binafsi.

Hii kama ilikuwa haijagunduliwa mapema, ilikuwa na hatari ya kusababisha upotevu kifedha za Yanga kulingana na kanuni za TFF/FIFA na ukilichimba suala hili kwa undani, kwa kufuata weledi. Kamwe hauwezi kusema yalikuwa ni makosa ya kibinadamu badala yake ni chuki ya kibinadamu ambayo haistahili kufanywa na kiongozi wa Klabu kubwa yenye heshima kama Yanga.

Zaidi, Katika hali nyingine, uamuzi wa Kamati ya Nidhamu uliandikwa na Gazeti la Uhuru na mwisho wa uchunguzi ulidhibitisha mtoa habari hizo alikuwa ni Tiboroha, akilenga kutaka kuuchafua uongozi wa Klabu, mchezaji mwenyewe dhidi ya jamii na kuusukuma uongozi kufanya uamuzi usio sahihi kwa faida zake yeye binafsi na si klabu.

1. 2. Aidha, EXCOM ilifanya uchunguzi wa ziada na kugundua vitendo, Tiboroha hakuweza kufikia malengo aliyekuwa ameyawekewa na EXCOM kwa kuwa zaidi alionekana kutaka kujiendeleza binafsi, kusikika peke yake na kujulikana mwenyewe kama “Mungu Mtu”, jambo ambalo lilichochea kelele ndani ya klabu kama vile yeye ni malaika:

∞ Angalia kiambatanisho (3), eti Mwenyekiti wa Matawi (nafasi ambayo haitambuliki kwenye katiba ya Yanga), amekuwa akiniagiza kubadili nafasi za waajiriwa, mfano ile ya (Tiboroha) ni lazima abaki kwa sababu mchango wake ni mkubwa na bila yeye hatuwezi kushinda au kufanya vizuri. Ukisoma barua yake utafikiri Tiboroha alikuwa akifanya kazi zake bure wakati anajua alikuwa ni mwajiriwa wa Klabu, tena kazi zake nyingi alikuwa akizifanya kwa kufuata “maagizo” anayopewa kama mwajiriwa.
Tayari kupinga kuondolewa kwake kumeanza kuripotiwa kwenye vyombo vya habari kama shinikizo la chinichini kupitia Msumi, huenda anafikiri kufanya hivyo inanitisha ili nibadili mambo kwa matakwa ya wasioelewa mamlaka ya Katiba. Naendelea kukumbusha Tiboroha alikuwa mwajiriwa anayelipwa mshahara (angalia kiambatanisho 4) huku mimi kama Mwenyekiti au Wajumbe wa EXCOM tumekuwa tukijitolea na kutolipwa hata posho.

∞ Ajabu Kichekesho zaidi, kila kizuri kilichokuwa kikifanyika, vyombo vya habari viliripoti kuwa ni kazi nzuri ya Tiboroha, lakini wakasahau kila zuri, yeye alikuwa ni mtekelezaji tu baada ya kuagizwa kutoka kwangu mimi mwenyekiti au baada ya ushauri wa kamati ya utendaji na baada ya hapo, yeye alipewa kibali cha kutekeleza jambo husika. Kila zuri lilikuwa lake, mabaya yakiwemo yale ya kuisaidia TFF kuiangamiza shingo ya Yanga, aliyeficha kapuni.

∞ Kuna taarifa kwenye vyombo vya habari ambazo zilithibitisha wazi kuwa Tiboroha alipania kujijenga binafsi kama Katibu Mkuu Bora zaidi kuwahi kutokea Yanga; hoja potofu kwa sababu wakati akiwa Katibu, hata mwalimu wa Klabu alifanikiwa kupatikana kwa ubingwa moja tu. Lakini akasahau kabla yake, Yanga ilishachukua ubingwa mara 24. Tena, propaganda ya kuwa yeye ndiye aliyeisaidia Klabu kusajili wachezaji wa kiwango cha juu zaidi huku akijua wazi kwamba wachezaji hao walikuwa ni pendekezo la Kocha Mkuu, huu ni uputofu wa hali ya juu kabisa.

¥ Ndani ya miezi yake 12 ya uongozi amechangia kushuka kwa kasi kubwa kwa mapato ya klabu huku matumizi ya klabu yakipanda mara nne zaidi kutoka Sh milioni 500 kwa mwaka hadi sasa takriban Sh bilioni 2. Kabla hajaja klabuni, tulikuwa tumekaribia kujikomboa na kuanza kujitegemea. Hii pia ni kwa yeye kukubaliana na ujinga wa kuitetea TFF ambayo mikataba yake, kwa kiasi kikubwa imeporomosha mapato yetu na kutuweka katika wakati mgumu kabisa, ajabu Tiboroha alikuwa upande huo.

3. Masuala ya kupotosha ya Tiboroha si mapya:
a. a. Wakati FIFA ilipoialika Yanga kwenye semina ya mafunzo iliyofanyika nchini Ghana, Tiboroha alijichagua mwenyewe asafiri kwa niaba ya Klabu bila kuitaarifa EXCOM, halafu akachukua “Cheti cha ugonjwa” na kukiwasilisha kwa mwajiri wake Yanga ili apate nafasi ya kusafiri kwenda nchini Ghana. Kujichagua yeye mwenyewe, ilikuwa ni kutofuata weledi.
a. b. Daktari (jina linahifadhiwa) aliajiriwa kwa ajili ya mechi dhidi ya MGAMBO likiwa ni pendekezo la Tiboroha, lakini baadaye Kamati ya Mashindano (baada ya kuwa imesababisha tatizo ndani ya Klabu), iligundua daktari huyo alikuwa ni mwanachama tena mwenye kadi wa Simba, akaondolewa’ pia.

a. c. Ngoma alipewa taarifa na Tiboroha kwamba anatakiwa kwenda kufanya majaribio na klabu moja nchini Uturuki. Tiboroha alifanya hivyo akijua Ngoma alikuwa anakwenda kushiriki michuano ya MAPINDUZI Cup, mbaya zaidi hakuwa amewasiliana na EXCOM kuhusiana na hilo kabla kumfahamisha mchezaji na kumpa taarifa hiyo. Baadaye kocha Kocha Mkuu, alilalamika kwamba kufanya vile ilikuwa ni kuondoa morali ya mchezaji katika michuano hiyo ya MAPINDUZI CUP na baada ya hapo, angekuwa akiwaza kuhusiana na Uturuki tu. Mwisho, kocha alisema, Ngoma alicheza chini ya kiwango katika michuano hiyo, akiamini Yanga inamzuia kusonga mbele kimaisha.
a. d. BDF ya Botswana ilianzima US$ 5,000/- ambazo hadi sasa hazijarejeshwa: EXCOM iligundua taarifa kuhusiana na deni hili, imekuwa ikifichwa na hakuna maelezo mrejesho kuhusiana hilo kutoka kwa Tiboroha ambaye amekuwa na ukaribu na wahusika kutoka Botswana.

a. e. Kuna mtu aliajiriwa kama Katibu Muktasi (PS) pamoja na mtu mwingine pia, lakini haikuidhinisha wala mwanasheria wa Yanga, hakutaarifiwa kuhusiana na hilo lilifanyika bila ridhaa ya EXCOM, badala yake alilifanya kwa kuwa anaona yeye ni mtu maarufu sana!

a. f. Hakufuata ushauri aliopewa na wataalamu wa TRA, hali iliyosababisha akaunti za Yanga kufungwa, hivyo mimi kulazimika kuanza kutoa fedha zangu za mfukoni katika uendeshaji wa Klabu kwa kipindi chote na wakati huo wachezaji walikuwa wakidai mishahara na tuko katikati ya msimu.
a. g. Alikuwa akitetea maslahi ya TFF na sio Yanga na kukubali kila TFF ilichokipendekeza. Mtu mwenye akili anaweza kufanya hivyo utadhani alikuwa mwajiriwa wa TFF na si Yanga? Hii inaonyesha hakuwa akifanya kazi kwa maslahi ya Yanga kama ilivyotakiwa, angalia katika masuala dhidi ya TFF, ukijumuisha.

a. h. Lile la kushindwa kumpigania msemaji Msemaji wa Klabu, Jerry Murro asifungiwe na TFF, huku akimchimba huku akijua alikuwa akipitia taarifa zote kabla ya Jerry kuzitoa. Alikuwa na roho mbaya kwa kuwa Jerry alipata umaarufu zaidi kwa wanachama kutokana na kuipigania klabu.
4. 4. Ukiangalia hayo juu, ni kati ya machache ambayo nimeona ninaweza kuyaanika kwenye vyombo vya habari, lakini yako mengi ambayo ni nyeti na haitakuwa sahihi kuyaanika kwenye vyombo vya habari kwa maslahi ya klabu. Yanga ilianza kung’amua mambo yanayomhusu Tiboroha muda sasa, alipoona mengi yamegundulika. Januari 14, 2016 aliandika barua kuomba radhi kwangu, akikiri kufanya makosa na kusema alikuwa akiyajutia. (angalia kiambatanisho 6)

4. 5. Sisi, hatukukubaliana na kutoa msamaha kutokana na hofu ya unafiki wake, na nilitoa ushauri; kwamba vizuri akachukua hatua ya kujiuzulu mara moja na huenda ingekuwa vizuri aeleze ana matatizo ya kifamilia pia kiafya, lengo lilikuwa ni kumpa nafasi ya kuachana na Yanga kwa amani pia kuilinda familia maisha yake huko mbeleni. Lakini nilimtaka ahakikishe zile fedha tunazowadai BDF kutoka Botswana, mara moja zinawasilishwa Klabuni na baada ya hapo, rasmi atakuwa amejiondoa.
4. 6. Tiboroha alikubaliana na hilo na kuandika barua ya kujiuzulu alioiwasilisha Januari 22, 2016 (angalia kiambatanisho 7)

4. 7. Pamoja na kumshauri ili ajiuzulu kwa heshima, lakini alionekana kuanza kutengeneza “Presha ya wanachama” kama vile mtu aliyeonewa. Kuna mkutano wa ujanjaujanja uliitishwa makao makuu ya Klabu, Tiboroha akiwa mshiriki mkuu nyuma ya pazia, hii ilikuwa ni Januari 23, 2016. Lengo ni kutengeneza hali ya hofu kwa Wanachama, jambo ambalo si sahihi. (angalia kiambatanisho 8)
7. Kwa yote hayo hapo juu:

a. a. Kamati ya Utendaji (EXCOM) inapenda kutoa taarifa kuwa imevunja mkataba wa Tiboroha kama Katibu Mkuu wa Yanga.

a. b. Klabu inatangaza, mara moja kuwa:
i. i. Baraka Deudeit atashikilia nafasi hiyo ya Katibu Mkuu wa klabu.
ii. ii. Omar Kaya atachukua majukumu yanayohusiana na wanachama wa klabu. Pia atahakikisha anasimamia mikutano yote ya matawi, kusaidia maandalizi ya uchaguzi ujao pamoja na masuala ya wanachama wapya.

iii. iii. Jerry Muro ataendelea kubaki katika nafasi ya msemaji wa klabu,
iv. iv. Faidhal Mike ni Mkuu wa Kitengo cha Fedha cha Klabu, akisaidiwa na Justina ambaye amepandishwa cheo na kuwa mhasibu mkuu msaidizi,
v. v. Klabu ipo katika kipindi cha kuboresha kitengo cha masoko cha klabu na hivi karibuni itatangazwa lakini kabla ya hivyo, Omar atashikilia kwa muda kitengo hicho.
vi. vi. Mwanasheria Frank Chacha kama mkuu wa kitengo cha Sheria Klabuni, yeye tunamuacha aendelee na mambo yake na masuala yote ya kisheria, klabu itayafanya kutumia wanasheria, nje ya klabu.

8. 8. Kuhusiana na uchaguzi na maneno ya kinafiki ya nungunungu ya chinichini kuwa eti ninaogopa uchaguzi; huku wakiwa hawajui kuwa katika maisha yangu sijawahi kushindwa uchaguzi: Ukweli mimi ndiyo nimekuwa nikusukuma kuitishwa kwa uchaguzi uitishwe ili nistaafu kupitia nafasi yangu ya uenyekiti. Nilimwaandika Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, kuitisha uchaguzi mara moja, akishindwa basi itabidi niivunje Kamati ya Uchaguzi na kuunda nyingine. (angalia kiambatanisho 9)
8. 9. Kutokana na kuuguliwa na baba yake mzazi, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi alishindwa kutekeleza hilo na akaamua kujiuzulu. (angalia kiambatanisho 10)

8. 10. Ikiwa ni sehemu ya majukumu yangu, kwa ushauri wa EXCOM niliomba kwao majina mapya ya Kamati ya Uchaguzi ili mchakato ufanyike (angalia kiambatanisho 11)
Hitimisho, nimegundua potofu ya kufikiri Tiboroha ni Katibu Mkuu wa kuchaguliwa, badala yake ni mwajiriwa wa kawaida ambaye aliingia mkataba kwa maslahi ya mapato yake. Tena kosa kumchukulia kama mtu ambaye amekuwa akitoa fedha zake za mfukoni kwa ajili ya kuendesha Klabu, mtu ambaye mimi nilipendekeza aajiriwe kama nililivyopendekeza kwa Mwalusako, Njovu, Mwesigwa, Maximo na wengine na nina mamlaka ya kuamua hatma ya mwajiriwa kulinda heshima na maslahi ya Klabu.

Kwa sababu mimi nimewekea dhamira ya uchaguzi ufanyike kwa haraka, huu unaweza ukawa wakati mwafaka wa wanachama kumpa Tiboroha imani ya kura zao ili awanie nafasi Mwenyekiti wa Klabu na wanipe uhuru wangu wa kuendelea na mambo yangu mengine, ambayo yapo karibu na moyo wangu kama vile kusaidi mandeleo ya Mbagala Kuu.

Katika maisha yangu, sijawahi kutanguliza au kupigania cheo, ndani ya Yanga maendeleo yanaonekana lakini wapo watu ndani ya Yanga wanaona mandeleo ipo kwake. Basi tuache demokrasia itawale; lakini na mimi nitatangaza kugombea tena nafasi hiyo, ingawa sidhani kama nitamaliza kipindi chote cha uongozi iwapo nitashinda kwa kuwa kutoka awali nilieleza Yanga kuwa yenye mafanikio ni katika Ligi ya Mabingwa Afrika lakini hilo halitawezekana bila ya Klabu kumiliki uwanja wake binafsi pale Jangwani.
Daima Mbele, Nyuma Mwiko
_____________
YUSUF MANJI
ANDIKA MAONI YAKO HAPA CHINI

Sunday, December 20, 2015

Picha: Diamond Platnumz Akiwa na Watoto Wote wa Zari

Kupitia kwenye mitandao ya kijamii mwanadada Zarinah Hassan ‘Zari the boss Lady’ ambaye ni mzazi mwenza wa mkali wa bongo fleva, Diamond Platinum alitupia picha hizi akiwa yeye, Tiffah na Diamond pamoja na watoto watatu wa zari ambao diaomond alimkutanao kuandika maeno kuashiria hiyo ndiyo familia.

Hii ni kwama mara ya kwanza kwa diamond kupiga picha na watoto hao wa zari tangu Diamond awe na mahusiano na mwanadada Zari.

Jionee picha hizo hapo chini

Monday, November 30, 2015

KIMENUKA..Miss Tanzania Atajwa Ufisadi wa Sh1.3 Trilioni

 Aliyekuwa ofisa mwandamizi wa benki ya Stanbic tawi la Tanzania, Shose Sinare amehusishwa na mipango ya kifisadi ambayo imeisababishia Serikali ya Tanzania hasara ya Sh1.3 trilioni kati ya mwaka 2012 na 2013.


Taarifa ambazo gazeti hili limepata kutoka Uingereza na hapa nchini, mwanadada huyo ambaye alikuwa mrembo wa Tanzania mwaka 1996, alishirikiana na aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bashir Awale.

Sinare hakupatikana kufafanua suala hilo ilhali Awale alifukuzwa nchini hivi karibuni.

Alipoulizwa jana kuhusu tuhuma hizo, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward Hosea alisema anatambua suala hilo,  linafuatiliwa na taasisi yake na hakutaka kutoa maelezo zaidi.

Taarifa kwamba Serikali imetumbukia katika kashfa nyingine kubwa ya ufisadi zimebainika baada Taasisi ya Uchunguzi wa Makosa Makubwa ya Ufisadi ya Uingereza (SFO) kuwasilisha mahakamani ushahidi wake kwamba kiasi cha Sh1.3 trilioni kilipotea wakati wa uuzwaji wa hati fungani za Serikali kwa benki ya Stanbic inayomilikiwa na Standard Group ya Afrika Kusini.

Mwanasheria wa SFO, Edward Garnier aliiambia Mahakama ya Southwark Crown ya jijini London, Uingereza inayosikiliza shauri hilo la kibiashara kwamba wakati wa mchakato wa benki kununua hati fungani Awale na Sinare walihusika.

Garnier alisema Awale alifukuzwa kazi Agosti 2013 baada ya kushindwa kutoa ushirikiano kwa timu ya uchunguzi ya ndani na Sinare alijiuzuru Juni 2013 na hivyo naye alifanikiwa kukwepa uchunguzi.

Katika uchunguzi huo, Garnier alisema maofisa hao waliwataka maofisa wa Serikali ya Tanzania wawapatie kwanza kiasi cha Dola za Kimarekani 6 milioni (Sh13 bilioni) ili waweze kufanikisha mkopo wa Dola 600 milioni (Sh1.3 trilioni) na ziingizwe kwenye akaunti za maofisa binafsi wa Serikali. Dola 6 milioni ni asilimia moja ya mkopo huo wa Dola 600 milioni. Garnier alisema mpaka sasa hakuna anayefahamu fedha hizo zipo mikononi mwa nani.

Hii ni mara ya pili SFO inafanikiwa kuibua ufisadi wa mabilioni ya dola kwa maofisa wa Serikali ya Tanzania baada ya ule wa mwaka 2002 ambapo maofisa waliongeza Sh73 bilioni katika bei halisi ya rada kutoka kampuni ya vifaa vya kijeshi ya Uingereza ya BAE Systems.

Watanzania walipopata habari hizo walipiga kelele maofisa waliohusika wachukuliwe hatua lakini Serikali ilikataa. Baadaye yalifanyika makubaliano maofisa wasishtakiwe na BAE pia isishtakiwe, lakini fedha zilirejeshwa nchini.

Katika shauri hili yanataka kufanyika makubaliano kama hayo ya awali kwamba Stanbic inayonilikiwa na kampuni ya Standard Group ya Afrika Kusini ambayo ni kampuni tanzu ya Industrial and Commercial Bank of China (ICBC) inatakiwa kulipa Dola 32.2milioni sawa na Sh69 bilioni, ikiwa ni pamoja na kuwalipa SFO Dola 16.0 milioni sawa na Sh36.3 bilioni. Pia inatakiwa kulipa faini ya Dola 6 milioni (Sh12.9) na riba Dola 1 milioni (Sh2.1bilioni) kwa Serikali ya Tanzania.

Zitto Kabwe

Akizungumzia sakata hilo, Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe aliitaka Serikali kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wote waliohusika na ufisadi huo.  Zitto, kupitia taarifa kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana alisema kati ya mwaka 2012/2013, Serikali kupitia Wizara ya Fedha iliuza hati fungani zenye thamani ya kiasi hicho cha fedha, ambapo dhamana za Serikali zilinunuliwa na benki ya Stanbic  inayomilikiwa na benki ya Standard Group ya Afrika Kusini.

“Hata hivyo, sehemu ya fedha hizo hazikuingia kwenye akaunti za Serikali ya Tanzania na pia gharama za bond (hati fungani) hiyo zilipaishwa kupitia wakala wa kati kati (middle men) na hivyo kupelekea rushwa ya takribani $60 milioni (Sh129 bilioni) kutolewa kwa maafisa waliothibitisha biashara hiyo,” alisema.

Stanbic

Hii itakuwa mara ya pili benki ya Stanbic kuingia katika mgogoro baada ya mwaka jana kutuhumiwa kupitisha kiasi kikubwa cha fedha kilichotokana na mgawa wa Sh306 bilioni kutoka Akaunti ya Tegeta.

Baadhi ya maofisa, mawaziri na watu maarufu waliopewa fedha zinazoaminika zilitoka Tegeta Escrow kupitia benki ya Mkombozi walijulikana na wakafikishwa katika Baraza la Maadili, lakini waliopokea fedha kutoka Stanbic hawajulikani ingawa uchunguzi uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) aligundua kwamba watu hao walichukua kwa mifuko ya sandarusi na plastiki.

Source:Mwananchi

Kimbunga cha Magufuli chatua Mashirika ya Umma, ATCL, TRL And Tazara Matumbo Moto

Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru amezitaka taasisi na mashirika ya umma nchini kuacha utegemezi kwa Serikali, badala yake kupunguza matumizi na wafanyakazi ili kuongeza mapato na ufanisi.

Mafuru alisema Serikali imebeba mzigo wa taasisi na mashirika hayo kwa kutegemea izipatia fedha kutoka Hazina kwa ajili ya kujiendesha, na kulipa mishahara ya wafanyakazi na kusababisha ufanisi wao kuwa mdogo.

Mafuru pia alitangaza kufuta posho za wabunge katika bodi za mashirika na kuanzisha mchakato wa kuwaondoa katika mashirika hayo, ili wabaki na jukumu lao la msingi la kuikosoa Serikali badala ya kuingia katika utendaji.


Kuhusu uzalishaji

Msajili huyo alisema inashangaza kuona kwamba mpaka sasa kuna mashirika ya umma ambayo bado yanaitegemea Serikali kulipa mishahara ya wafanyakazi wake.

Aliyataja mashirika hayo kuwa ni Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Kampuni ya Hifadhi za Reli (RAHCO) na Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (Tazara).

Alisema hakuna haja kwa Serikali kuendelea kuwa na mizigo hiyo isiyozalisha ikiwamo kubeba gharama za kuendesha mashirika hayo.

“Wenyeviti na wajumbe wa bodi, pamoja na watendaji wakuu wa kila shirika mkae chini mjitafakari, kwa nini muendelee kuongoza mashirika hayo wakati mmeshindwa kuzalisha. Rais ameniagiza kuwakumbusha kwamba mrejee malengo ya kuanzishwa kwa taasisi zenu,” alisema.

Mafuru alisema taasisi ambazo uzalishaji wake umeshuka lakini gharama za uendeshaji ziko juu, hazina budi kupunguza wafanyakazi ili kulingana na mapato yake.

“Kama hawataweza kufanya hivyo, watafute njia nyingine ya kuongeza uzalishaji kwa kutumia wafanyakazi walionao. Kwenye sekta binafsi, kampuni ikianza kufanya vibaya inapunguza matumizi yake na moja ya njia wanazotumia ni kupunguza wafanyakazi. Huku serikalini utasikia mtendaji mkuu akiandika barua, siyo proposal (mradi), kuomba fedha kwa ajili ya mtaji. Hatuwezi kwenda mbele,” alisema.

Mafuru aliyasema hayo jana katika mkutano maalumu ulioitishwa kwa maagizo ya Rais John Magufuli ili kuwakumbusha watendaji mbalimbali wa taasisi na mashirika ya umma nchini, juu ya wajibu wao katika kuwahudumia wananchi.

Mkutano huo uliwahusisha wenyeviti wa bodi, wajumbe wa bodi na watendaji wa taasisi na mashirika mbalimbali ya umma ambayo kwa sasa yamefika 216, yakiwa na mali zenye thamani ya Sh20 trilioni.

Hata hivyo, alisema pamoja na mtaji huo, taasisi na mashirika ya umma yamekuwa yakichangia Sh185 bilioni kwenye Pato la Taifa.

“Kwa mtaji wa Sh20 trilioni, hicho ni kiasi kidogo sana ambacho kinarudi serikalini. Kwa wenzetu wa sekta binafsi, ukimpatia mtaji huo basi baada ya muda fulani unamkuta kapata mara mbili ya mtaji aliopewa,” alisema Mafuru ambaye amefanya kazi kwenye taasisi za benki kwa miaka 15.

Alisema Rais Magufuli amemtuma kuwakumbusha kila mmoja kwenye taasisi yake ahakikishe anapunguza kero zote zinazopatikana kwa kutumia rasilimali alizonazo.

Alisisitiza kuwa kila mmoja atambue kwamba anawajibika katika kuleta maendeleo ya Taifa hili.

Msajili huyo aliongeza kuwa Serikali imekuwa hainufaiki na mashirika ya umma ambayo ndiyo yangekuwa msaada mkubwa wa kupunguza mikopo ambayo inadaiwa.

Hata hivyo, alisema mashirika yamekuwa yakiiacha kulipa madeni hayo licha ya kwamba yanapata faida kubwa kila mwaka.

“Siyo lazima faida inayopatika kwenye taasisi na mashirika ya umma irudi serikalini, lakini mashirika yenyewe yanaweza kusaidia katika shughuli mbalimbali za maendeleo ambazo Serikali ilitakiwa kufanya” alisema.

Mafuru alitoa mfano wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) akisema linapopata faida kubwa, linaweza kuamua kujenga kipande cha reli kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro na kuisaidia TRL na Serikali.



Wabunge kutopewa posho

Mafuru alisema wabunge ambao ni wajumbe wa bodi za mashirika hayo, hawatalipwa posho za vikao vya bodi kwa sababu wanalipwa posho hizo kwenye kamati zao.

Alisema kuendelea kufanya hivyo ni sawa na kuwalipa posho mara mbili kwa kazi moja, jambo ambalo halikubaliki.

Alisema kuna mpango wa kuwaondoa wabunge kwenye bodi hizo ili washiriki kikamilifu kuisimamia Serikali na kwamba mbunge anapokuwa sehemu ya bodi anakosa uhuru wa kufanya kazi yake kama mwakilishi wa wananchi.

“Shirika linapofanya vibaya wajumbe wote wa bodi wanahusika bila kujali ni mbunge au la. Kuna mbunge mmoja alipata msukosuko wakati wa sakata ya Tanesco, kwa hiyo tunajaribu kuwalinda ili wafanye kazi yao kikamilifu,” alisema.

Kuhusu uteuzi wa wenyeviti wa bodi, Mafuru alisema Rais anawateua kwa sababu anaamini wana uwezo wa kusimamia na kuongoza bodi hizo ili kuleta matokeo chanya.

Alisema wenyeviti wengi wamekuwa wakichukulia nafasi wanazopewa kama zawadi na kushindwa kusimamia majukumu ya mashirika au taasisi husika.

Alisisitiza kuwa uenyekiti ni jukumu kubwa ambalo linahitaji kuifahamu taasisi vizuri ili kutoa maamuzi sahihi.

Aliwataka wenyeviti wa mashirika ya umma kutambua wajibu wao na kuondokana na dhana kwamba wanapoteuliwa basi wanapewa ‘ulaji’.

Kwa upande mwingine aliyataka mashirika hayo kufanya ukaguzi wa hesabu zao na kuwasilisha ripoti katika ofisi yake.

Akitoa maoni yake kuhusu uendeshaji wa mashirika ya umma, Mkuu wa Taasisi ya UsiMamizi wa Fedha (IFM), Profesa Emmanuel Mjema, alisema Wakala wa Manunuzi ya Serikali (GPSA) amekuwa tatizo ambalo linapaswa kuangaliwa. Pia, alisema Wakala wa Huduma za Ufundi na Umeme (Temesa), nao wamekuwa ni tatizo kwa kutopeleka magari kwa ajili ya kufanyiwa matengenezo huku wakitoza fedha, lakini wanaambiwa wapeleke magari hayo GS Motors.

Mafuru alisema amepokea maoni hayo na kuongeza kuwa ofisi yake imekuwa ikipata malalamiko kutoka mashirika mbalimbali kuhusu GPSA na kuahidi kufuatilia na kuyapatia ufumbuzi wa kudumu.

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Albina Chuwa alitaka mishahara ya watendaji wa taasisi na mashirika ya umma iangaliwe upya kwa sababu wapo wanaopata mikubwa kiasi cha Sh36 milioni wakati wengine wanapokea Sh3 milioni.


Je Kasi ya Magufuli na Watendaji Wake Ndio Mwanzo wa Udikteta? Ama ni Kasi Inayotakiwa Katika Taifa Hili ?



Mwalimu Nyerere once a time alisema kama nigetaka kuwa dicteta ningeweza. hivi sasa watanzania tumepata upofu wala hatuoni tena. nimewahi kusema kwenye post zangu kuwa IPO siku watanzania watamkumbuka Rais Kikwete.

kwanini niseme ivo, twende pamoja na kama unamatongotongo kanawe,na kama umemeza viroba kaa mbali na hii post,only great thinkers.

1. VITISHO NA HOFU
ukubali au ukatae magufuli sasa anaogopwa na amejaza hofu wananchi haswa wafanyakazi na wafanyabiashara. kumbekeni Adolph Hitler alishinda uchaguzi wala hakupindua serikali pia alipata public sympathy hata pale alipokesea. tazama sasa hata hii post kuna watu watakosoa bila kujali relevance yake.

2. KUVUNJWA KWA HAKI ZA BINADAMU.
hivi sasa unaweza kuweka polisi bila kushtakiwa mfano. hivi jeuri ya Paul Makonda yakumweka MTU kizuizini bila kumpeleka mahakamani ni uvunjaji wa haki za binadamu. sasa ivi kila mkuu wa wilaya anaamua tu kwa ubabe hats bila kuangalia haki za binadamu.

3.KUVUNJWA KWA UTAWALA WA SHERIA.
KUNA uvunjaji wa sheria wazwazi huku wananchi wakichekelea. mh magufuli binafsi alidai atavunja nyumba ambayo inazuia bomba la maji hata km kesi IPO mahakamani kisha watu wanachekelea hii no hatari. kuna bomoa bomoa ambazo zinaendelea hata km kuna pingamizi la mahakama zinavunjwa tu kwa jeuri. pia polisi mwanza walivunja sheria kuzuia kuagwa kwa mawazo.chekeleeni lakini lilikufika u will understand the rule of law what does it mean?. kuna mkuu wa wilaya geita amefukuza kaxi daktari bila kufata utaratibu wa Sheriakupitia kwa mwajiri yani mkurugenzi. OK just laugh and enjoy but it will b u one day

4.UBABE NA JEURI.
BAADJI ya viongozi sasa wamejawa na ubabe na jeuri ambayo ni sifa ya madikteta. hatuitaji viongozi wababe. tunataka mifumo iliopo wazi kuanzia mtaani hadi wilayan km sio taifa. MTU anawezeje kufuta likizo ya mtumishi ambayo ni haki yake km so jeuri na ubabe nothing else u can say.

Conclusion.
Naomba tuangalie mifumo ya uongozi na utawala wa nchi yetu. kuliko magufuli kuwafukuza watu kila siku tatizo sio watu ni mfumo. napendekeza katiba mpya ipigiwe kura ili ianze kutumika. tuache ubabe na vitisho. Magufuli asipowekewa check n balance na kamati kuu believe m he will be a dictator .

By  Assadsyria3

Sakata la Makontena: Mwigulu, Saada Mkuya, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Wanatakiwa Wawe Ndani

Ni jambo la kusikitisha kuwepo upotevu wa kiasi kikubwa cha pesa kwa ukwepaji kodi wa makontainer 349 yenye thamani billion 80 wakati wenye dhamana ya kulinda mali hizi zisipotee wakina Mwigulu Nchemba, Saada Mkuya, Katibu Mkuu wizara ya fedha wakiwa nje bila kuchukuliwa na hatua yoyote kama walivyo wenzao sita walioachishwa kazi na kuwekwa chini ya uchunguzi, haiwezekani makontiner idadi kubwa kama hii ipotee billa wakuu hawa kujua lolote, tunaiomba serikali iwafuatilia na kuwawajibisha mara moja, hivyo hivyo katika uongozi wako Mh. Tingtinga untakiwa kuwafyeka wote. Vivyo hivyo tnataka taarifa sahii ya maandishi kuonyesha kama fedha zlizoamriwa kulipwa kutoka kwa wana-ESCROW kama zimelipwa kwa wakati.
Jamii Forums

Taarifa Kutoka Azam Kampuni ya Bakhresa Kuhusu Kuhusishwa Kwnye Makontena 349 Yaliyotolewa Bandarini Bila Kulipiwa Ushuru

Kumekuwa na taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa kampuni ya Bakhresa inahusika na upotevu wa Makontena 349 yaliyoripotiwa hivi karibuni kuwa yametolewa bandarini bila kulipiwa ushuru. Taarifa hizo zilitolewa na Waziri Mkuu wakati wa ziara yake ya Bandari ya Dar es salaam hivi karibuni.
Uchunguzi wetu umeonyesha kuwa si kweli kuwa kuna makontena yenye bidhaa zilizoingizwa na kampuni hio ama ni miongoni mwa makontena yaliyohusika katika sakata hilo. Isipokuwa kumetokea upotevu wa makontena yaliyoingizwa nchini na baadhi ya wafanyabiashara katika eneo la kuhifadhia makontena(ICD) linalomilikiwa na kampuni hiyo la Azam ICD.
Aidha imebainika kuwa kuna uchunguzi unaofanywa na mamlaka ya mapato nchini TRA, huku kukiwa na ushirikiano na uongozi wa Kampuni hiyo (SSB Group of Companies) kuhakikisha wale wote wanaohusika na upotevu huo wanachukuliwa hatua na kodi yote ya serikali inalipwa na wamiliki wote wa makontena yaliyohusika katika upotevu huo wanawajibishwa.

SSB Group of Companies

Corporate Affairs Department

November 29, 2015

Waziri Mkuu: Tumedhamiria Kuwatumikia Watanzania...Tutahakikisha Mapato Ya Taifa Yanatumika Kwa Maslahi ya Watanzania Wote

WAZIRI MKUU Majaliwa Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuhakikisha kila kinachokusanywa kama mapato ya nchi kinatumika kwa maslahi ya Watanzania wote na si kwa manufaa ya wachache.
Alitoa kauli hiyo jana mchana (Jumapili, Novemba 29, 2015) wakati akifunga maadhimisho ya miaka 20 ya Dayosisi ya Pwani ya Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) kwenye ukumbi wa PTA, viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

“Serikali imeanza kukabiliana na upotevu wa mapato ya Serikali na kuepuka matumizi yasiyo ya lazima ya fedha za umma. Nia yetu ni kuhakikisha kila kinachopaswa kukusanywa kama mapato ya nchi, kikusanywe na kitumike kwa masuala ya msingi kwa ustawi wa Watanzania wote na si kwa watu wachache,” alisema.

Akifunga maadhimisho hayo kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu alisema Serikali imedhamiria kupambana na maovu yote na kuondoa kero zinazowaumiza wananchi wa kawaida.
 “Wako watu wanaoamini kwamba hatuwezi, nawaomba waondoe hiyo dhana. Wako watu wanaodhani kwamba kwamba utawala huu ni wa watu wapole, nao pia waondoe hiyo dhana,” alisema huku akishangiliwa na mamia ya waumini waliohudhuria sherehe hizo zilizoanza Novemba 27, 2015.

“Tunawaomba Watanzania wote mtuunge mkono kwenye vita hii na mtuwezeshe kuifanya kazi hiyo. Tunaomba waumini wote mtuombee katika sala zenu za kila siku ili tuweze kuongoza kwa haki na kuwaletea Watanzania wote maendeleo,” aliongeza.

Akinukuu kitabu cha Mithali sura ya 29 mstari wa pili, Waziri Mkuu alisema: “Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi, bali mwovu atawalapo, watu huugua. Mtuombee viongozi wenu tuwe waadilifu na wenye kutenda haki. Nasi tutaendelea kuwa waadilifu ili watu wetu wasigue,” alisema.

Aliwataka viongozi wa kanisa hilo waendelee kuisaidia Serikali katika kujenga kundi la watu wenye maadili mema ili walisaidie Taifa kuwa na watu waadilifu na hivyo kupunguza kero nyingi zinazoikabili jamii.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na waumini wa kanisa la hilo kutoka mikoa mbalimbali, Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT, Askofu Silas Kezakubi alisema Kanisa hilo litaendelea kumuombea Rais Dkt Magufuli na viongozi wenzake ili wawe na afya njema, wawe na hekima na kuahidi kwamba wataendelea kuwaweka chini ya ulinzi wa Mungu siku zote.

Alisema wao kama kanisa wanaamini kwamba Serikali ya awamu ya tano ina nia ya kuwatumikia wananchi kwa bidii na uadilifu lakini akasisitiza kuwa siri ya bidii na uadilifu inapatikana kwenye neno la Mungu.

Akisoma risala ya kanisa hilo, Askofu wa AICT Dayosisi ya Kibaha, Askofu Charles Salalah alisema kanisa halina budi kushirikiana na Serikali kwa sababu wote wanawahudumia watu walewale isipokuwa katika malengo tofauti.

Alisema kanisa hilo linahubiri maadili mema na bidii katika kazi kwa vile linaamini kuwa maendeleo hayadondoki kutoka juu wala hayaoti kama uyoga bali yanapatikana kwa watu kufanya kazi.

Akisisitiza kuhusu uadilifu, aliwataka wazazi kudumisha ndoa zao ili watoto wapate malezi mema kutoka kwa baba na mama na kwamba baba na mama wasipokaa vizuri, watoto hawawezi kuwa waadilifu.

“Wazazi tunao wajibu wa kupanda mbegu bora ya uzalendo kwa watoto wetu. Endapo tutapanda mbegu mbaya ya kuwagawa watoto wetu kwa itikadi tofauti, ni lazima tujue kuwa tutavuna tunachopanda.”

“Tukumbuke kuwa tunalo Taifa moja tu la Tanzania. Hata kama watoto wetu watakuwa na upenzi na vyama vyao, ni lazima tuwalee katika misingi ili wakue wakijua Taifa letu ni moja tu. Ndiyo maana tunaweka mkazo kwenye familia kwa sababu maadili mema yanaanzia nyumbani,” alisisitiza.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMAPILI, NOVEMBA 29, 2015.

M/Kiti CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe akifatana na alikuwa mgombea urais wa chama hicho Mhe. Edward Lowassa pamoja na viongozi mbalimbali wakitazama eneo ambalo Alphonce Mawazo alifanyiwa kitendo ya kinyama cha kukatwakatwa mapanga na watu wanaosemekana ni wafuasi wa CCM ikiwa ni umbali mchache kutoka kutuo cha polisi na ofisi za CCM katika barabara kuu inayoelekea Geita kutokea Busanda.

Moto Wa Magufuli Watua Kwa Bakhresa.......TRA Yazuia Makontena Yake Bandari Kavu, Kampuni Yake Yahusishwa na Ukwepaji Kodi


KAMPUNI ya Said Salim Bakhresa (SSB) inachunguzwa na vyombo vya dola kwa tuhuma za kushiriki kukwepa kodi na hivyo kuikosesha serikali mabilioni ya fedha kutokana na makontena yaliyohifadhiwa kwenye bandari yake ya nchi kavu (ICD) ‘kupotea’ bila kulipiwa kodi.

 Tayari Mamlaka ya Mapato (TRA) imepiga marufuku SSB kuingiza makontena katika bandari hiyo kavu ambako ndiko kunadaiwa kufanyika kwa vitendo hivyo vya ukwepaji wa kodi kutokana na baadhi ya makontena kupotea katika mazingira ya kutatanisha.

Katika barua iliyoandikwa kwenda kwa Meneja Mkuu wa SSB iliyosainiwa na Wolfgang Salia kwa niaba ya Kamishna wa Ushuru na Forodha wa TRA, inaeleza kuwa usitishwaji huo unatokana na kampuni hiyo ya Bakhresa kuchunguzwa kwa tuhuma za kuwepo madai ya kujihusisha na ukwepaji wa kodi kwa baadhi ya kontena zilizoingia na kutoka kwenye ICD yake.

Kwa mujibu wa barua hiyo, vitendo hivyo vya ukwepaji wa kodi vimefanywa kinyume cha Sheria ya Ushuru wa Pamoja wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Mwaka 2004 na hivyo kuikosesha Serikali mapato.

“Unafahamu kwamba uondoaji wa bidhaa kutoka eneo linalodhibitiwa na forodha, ambalo kodi na ushuru wa serikali haujalipwa ni kinyume na sheria kwa mujibu wa Sheria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Usimamizi wa Forodha ya mwaka 2004 na kanuni zake kwa vile husababisha upotevu wa mapato ya Serikali.

“Kwa sababu hiyo, imeamuriwa kukuzuia kupeleka makontena katika bandari yako kavu kuanzia tarehe ya barua hii, hadi suala hili litakapotatuliwa. Pande zote zinazohusika zinapaswa kutii amri hii.

“Kutokana na sababu hizo, tunasimamisha upelekaji wa makontena katika bandari yako kavu. Usitishaji unaanza mara moja. Hata hivyo utoaji wa bidhaa zilizopo katika bandari hiyo tajwa utaendelea,” ilisema sehemu ya barua hiyo iliyoandikwa Novemba 17, mwaka huu.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Walipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo alipoulizwa juu ya suala hilo jana, alikiri kampuni hiyo kuchunguzwa, lakini akagoma kuzungumzia kwa undani kwa kuwa suala hilo liko kwenye uchunguzi.

“Mimi siwezi kulizungumzia suala hilo kwa sababu liko kwenye uchunguzi na wanaofanya uchunguzi huo ni state organ (vyombo vya dola). Katika hatua hiyo, mimi siruhusiwi kusema lolote,” alisema Kayombo.

Meneja wa Kundi la Makampuni ya Said Salim Bakhresa, Said Mohamed alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, alisema yeye hahusiki na masuala ya ICD badala yake mambo hayo aulizwe Meneja wa ICD aliyemtaja kwa jina moja la Khan. “Mimi niulizie unga umekosekana... Sihusiki kabisa na mambo hayo,” alisema Mohamed.

Hata hiyo, Mohamed aligoma kutoa mawasiliano ya Khan, akisema: “Hiyo namba mimi hapa sina, wewe mtafute tu huko ICD atakupa maelekezo zaidi.”

Habari zilizopatikana jana pia zilieleza kuwa mmoja wa wafanyakazi wa SSB anayeishi maeneo ya Kinyerezi (jina tunalihifadhi), alivamiwa na kundi la maofisa wa Serikali kuanzia asubuhi hadi jioni na kufanya upekuzi kwake.

“Tangu asubuhi hawa jamaa wamekuja hapa wakamchukua mjumbe wa eneo hili na kwenda naye kufanya upekuzi, hadi sasa hivi wanaendelea kufanya kazi hiyo,” alisema Tito Bagule, mkazi wa eneo hilo.

Tayari Rais John Magufuli ameshamsimamisha Kamishna Mkuu wa TRA, Rished Bade kutokana na tuhuma za uzembe na rushwa na kusababisha upotevu wa makontena zaidi ya 349 yenye thamani ya Sh bilioni 80.

Upotevu huo umegundulika baada ya makontena hayo kuonekana kwenye mifumo ya Mamlaka ya Bandari, lakini haimo kwenye mifumo ya TRA.

Kabla ya kusimamishwa kazi, Bade alikiri kupotea kwa makontena hayo, wizi ambao alisema unafanywa kati ya bandari kuu na bandari kavu (ICD) ya Ubungo.

Alisema kutokana na upotevu wa kontena hizo mmiliki wa bandari hiyo ameamriwa kulipa faini ya Sh bilioni 12.6 na hadi sasa alishalipa Sh bilioni 2.4.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Diwani Athuman, amesema tayari jeshi hilo limeanza upelelezi kuhusu kashfa ya upotevu wa makontena iliyobainishwa hivi karibuni na kusababisha baadhi ya vigogo wa TRA kusimamishwa kazi.

Pamoja na upelelezi huo, alisema wameanza uchunguzi wa mali za wafanyakazi wote waliohusishwa na kashfa mbalimbali TRA kama ilivyoagizwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ili kubaini kama zinaendana na kipato chao halisi.

 Akizungumza na mwandishi wetu jana, Diwani alikiri kuwa jeshi hilo linawashikilia watumishi wanne kati ya watano wa TRA ambao jeshi hilo liliagizwa liwakamate na kuwahoji kuhusu sakata la upotevu wa kontena 349.

“Tuliagizwa tuwakamate watumishi watano, mpaka sasa tumewakamata wanne, mmoja ndio tupo kwenye utaratibu wa kumkamata, lakini kikubwa ni kwamba tumeanza upelelezi, kama tulivyoagizwa,” alisisitiza DCI Diwani.

Zitto Afunguka..Asema Nguvu ya Lowassa ilikuwa Kubwa Sana Kiasi cha Kuwavurugia ACT Wazalendo Katika Uchaguzi

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema nguvu ya aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa ilivuruga mpango wake wa kupokea wabunge 50 kabla ya Uchaguzi Mkuu.

Alisema Lowassa aliyekuwa akiungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) alikuwa na nguvu kubwa kiasi cha kufanya ACT pia ishindwe kupata wabunge wengi katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika nchini Oktoba 25.

Zitto alitoa kauli hiyo alipotakiwa kueleza sababu za ACT kushindwa kutimiza azma yake ya kupokea wabunge 50 kutoka vyama mbalimbali, kabla ya Uchaguzi Mkuu na kupata wabunge wengi baada ya uchaguzi huo kama alivyoahidi miezi michache kabla ya kuanza kwa kampeni.

Alibainisha kuwa chama chake kilifanya mazungumzo na wabunge wengi waliokuwa CCM na Chadema ambao walikubali kujiunga nacho na kushiriki uchaguzi kupitia chama hicho. Lakini mpango huo ulibadilika baada ya Lowassa kujiunga na Chadema na baadaye kuwania urais akiungwa mkono na Ukawa.

“Wabunge wengi walikubali kuungana nasi, wamo wa CCM na wabunge wa upinzani… lakini upepo wa Lowassa uliwabadilisha na hili tusingeweza kulidhibiti kwa kipindi kile,” alisema Zitto na kuongeza kuwa:

“Katika mazingira ya kawaida Lowassa ndani ya Chadema ni watu wachache sana wangekwepa upepo wake. Kwanza haikutegemewa kuwa (Lowassa) anakwenda wapi. Wapo walioamini kuwa anakuja kwetu (ACT), lakini ukweli ni kuwa hatukuwa na mazungumzo kati yetu (ACT) na Lowassa, ingawa kulikuwa na wish (matakwa) ya kuwa na coalition (umoja) kubwa zaidi ya kuunda kambi ya upinzani.”

Kwa nini ACT haikujiunga Ukawa
Zitto alisema sehemu kubwa ya waliounda ACT walitoka Chadema, hivyo kulikuwa na mazingira magumu ya kufanya kazi pamoja tena.

“Sisi tuliweka sharti moja, katika mazingira yoyote ya kufanya kazi pamoja, kwa matokeo yoyote yatakavyokuwa, moja ya ajenda ilikuwa kurejesha miiko ya uongozi jambo ambalo wenzetu hawakuwa tayari kutangaza mali,” alisema Zitto.

Lakini, mwisho baada ya majadiliano, ACT waliona kwa chama hicho ambacho kinaanza, kikiingia kwenye muungano na vyama vikubwa kingeweza kumezwa hivyo ni vizuri kwenda wenyewe ili wapate fursa ya kujitangaza kwa kuweka wagombea katika kila jimbo.

Ulikuwa uchaguzi wa ovyo
Akitoa maoni yake kuhusu uchaguzi uliopita, Zitto alisema ulikuwa mgumu, usioeleweka na uliokosa ajenda za wananchi. Badala yake, ulilenga mapambano ya wagombea na si sera.

“Uchaguzi ulikuwa kati ya CCM na Ukawa, ulikuwa ni kati ya (John) Magufuli na (Edward) Lowassa. Ulikuwa kuhusu personalities (watu) na siyo issues (hoja), naweza kusema ulikuwa miongoni mwa uchaguzi wa ovyo kweli kuwahi kutokea nchini,” alisema Zitto.

Aliongeza kuwa uchaguzi wa mwaka huu ulikuwa tofauti na wa miaka ya nyuma kutokana na kuwa wagombea wote wenye nguvu walikuwa ndani ya mfumo.

“Usingeweza kuwatofautisha wagombea wote waliokuwa au waliotokana na mfumo uliopo… ilikuwa vigumu kuacha kumfananisha mgombea wa CCM na yule wa Ukawa, wote ni walewale usingetegemea chochote. Kwa hiyo sisi (ACT) hata tungejitahidi tusingeweza kufanya kitu ni mara chache sana tulikuwa tukisikika,” alisema.

Kwa mujibu wa Zitto, uchaguzi uliopita ulikuwa mgumu na usio na ajenda ikilinganishwa na wa mwaka 2010.

“Kumbukeni uchaguzi wa mwaka 2010, vyama vilibishana kuhusu ajenda, baada ya uchaguzi watu walikuwa na ajenga ya uchaguzi, lakini angalia sasa wapinzani au vyama wanajadili nini, hakuna,” alisema.

Alisema ajenda ya kupinga ufisadi na rushwa iliyokuwa ikitumiwa na wapinzani, sasa imechukuliwa na Rais Magufuli.

“Sasa watu wanasubiri kusikia Rais atasema nini, watu wamesahau kwamba hakuna Baraza la Mawaziri, lakini nchi inakwenda… hata ile hoja ya Ukawa ya kutomtambua Magufuli haipo tena,” alisema.

Upinzani umepoteza
Zitto anasema anachokiona ni wapinzani umepotea kutokana na ajenda yao ya ufisadi kuchukuliwa na Rais Magufuli.

“Sasa unasikia Magufuli anakuwa mkali sana kuhusu rushwa na ufisadi jambo ambalo zamani halikuwapo naweza kusema tumebadilishana. Zamani ilikuwa wapinzani wanazungumzia rushwa na CCM wanaitetea Serikali, lakini sasa majukumu yamebadilika,” alisema.

Alisema kwa sasa sauti ya wapinzani katika hoja haisikiki na badala yake anasikika Rais Magufuli pekee ambaye amekuwa Serikali na upinzani wakati mmoja.

“ Hii itaimarisha zaidi demokraia kwa sababu kwa muda mrefu upinzani umekuwa ukitegemea matukio kujenga au kufanya siasa, itabidi sasa upinzani uendane na hoja katika siasa… lakini mwisho wa siku tunaangalia mwananchi anafaidika na nini? ” alihoji.

Nafasi ya wapinzani siasa za Tanzania
Zitto alisema kwa ujumla wapinzani wameanza vizuri kwani licha ya kuwa anachofanya Rais Magufuli kuhusu rushwa kinaonekana kukonga nyoyo za Watanzania, ukweli unabaki kuwa CCM imechokwa.

“Upinzani una wabunge wengi sana ndani ya Bunge, 122, kwahiyo tunaweza kujipanga na kufanya kazi ya kuionyesha Serikali matatizo yake wakati wote na hiki ndicho tulichokuwa tukifanya…Lakini tunayoiona sasa hivi ni kuwa hatujui, je, nguvu ya Magufuli, ni yake peke yake au ni nguvu ya taasisi? Na kama ni yake CCM itakuwa ni ile ile na mashambulizi dhidi ya CCM yatakuwa yaleyale,” alisema.

Mtazamo wake kwa Rais Magufuli
Zitto anamwona Rais Magufuli kama kiongozi aliyekosa msingi, kwani alichaguliwa bila makundi, hivyo kila anachofanya kinapaswa kuwafurahisha wananchi ili apate kuungwa mkono.

Alisema kwa muda mrefu wabunge walionekana kuwa na nguvu kwa kuwa pale Bunge lilipokuwa likipambana na Serikali, wananchi walikuwa nyuma ya Bunge, lakini sasa hali inaweza kuwa tofauti.

“Kwa namna ya uongozi wa Magufuli, Bunge linaweza kukosa nguvu kwani likijaribu kumkwamisha atatetewa na wananchi. Wakimpinga (Magufuli) wananchi watawapinga (wabunge). Na Magufuli alivyo anaweza kusema turudini kwenye uchaguzi, maana akivunja Bunge tunarudi kwenye uchaguzi kwani ana uhakika yeye atashinda, lakini wabunge hawatakubali kuingia kwenye gharama za uchaguzi tena.”

Tutampima Magufuli kwa posho
Wabunge wanataka kukopeshwa Sh 130milioni badala ya Sh90milioni, je Zitto anasemaje?

“Tumuangalie, Je, atasalimu amri kwa shinikizo la wabunge la kuongezewa mkopo wa gari au atatia mguu kwenye kiasi ambacho wabunge walilipwa mwaka 2010… akisalimu amri ina maana ni mtu ambaye atataka ushirikiano na Bunge, lakini akitia mguu ina maana ana msimamo,” alisema na kuongeza: “Wabunge huwa wanakimbilia kusema tutazuia bajeti, Je, atatishika. Bado tuna muda wa kutosha wa kuweza kumsoma Magufuli na kuona ni jinsi gani wanakwenda.”

Kuna uamuzi ambao tayari ameanza kuhusu kurejesha mashamba ambayo hayajaendelezwa, lakini lipo suala la viwanda. Je, anafanya nini kuhusu nguo kutoka nje, kuna ukwepaji mkubwa sana wa kodi na viwanda vya Tanzania,

Zitto anaenda mbali kwa kusema kwa Rais wa aina ya Magufuli ni lazima kuwe na namna ya kumdhibiti kwani Watanzania watajikuta wanatengeneza ‘dikteta’.

Alisema ili kuendana na kasi ya kiongozi huyo wa nchi, inatakiwa kuwa na Bunge imara.

“Bunge ni lazima libadilike, liache kushambulia watu na badala yake lijikite kwenye hoja na kwa jinsi Magufuli alivyo wapo wabunge wengi wataathirika na maamuzi yake… wapo wabunge ambao wapo kwenye matukio ya rushwa, wafanyabiashara ambao wataguswa na maamuzi yake, kwa hiyo kwa mwaka mmoja tutashuhudia mengi, ” alisema.

Zari wa Diamond na Mama Diamond ni Vita Kwa Kwenda Mbele....Mama Hamtaki Mkwe, Zari Atoa Masharti

NI vita! Baada ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwenda nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ kumwangukia mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari’ kufuatia kuwepo kwa figisufigisu kati yao huku mama wa msanii huyo, Sanura Kassim ‘Sandra’ akihusishwa, mazito yameibuka.

TUJIUNGE NA CHANZO
Habari kutoka chanzo cha ndani ya familia ya Diamond zinamwagika kwamba, Zari amekubali kuja Bongo lakini akatoa sharti: “Nakuja Bongo, Desemba 8, lakini mama (mama mkwe) aondoke pale nyumbani (Tegeta-Madale, Dar).”

ZARI ATIA NGUMU, AKUBALI
Chanzo hicho kilimwaga ‘ubuyu’ kwamba, awali Zari alimtilia ngumu Diamond lakini baadaye alikubali kurejesha amani kama ilivyokuwa zamani hivyo watakuja wote Bongo baada ya kujiachia vya kutoka huko Sauzi nyumbani kwa mwanadada huyo.


DIAMOND KICHEKO SAUZI
Kuhusu kuweka mambo sawa na kuwa atarejea Bongo na Zari na mtoto wao, Latiffah ‘Tiffah’, Diamond alilidokeza gazeti hili kwamba, sasa ni ‘full’ kicheko na anamshukuru Mungu kwa kufanikisha kufanya mambo kuwa kama mwanzoni.
Alitamba kuwa atatinga Bongo wiki hii au mapema wiki ijayo akiambatana na familia yake kwani kwa sasa wapo poa na hakuna manenomaneno tena.
“Nakuja na familia yangu. Kwa sasa tupo poa sana na maisha yanaendelea. Kiukweli huku South (Sauzi) tuna amani sana,” Diamond aliliambia gazeti hili wikiendi iliyopita.

TURUDI KWA CHANZO BONGO
Ilidaiwa kwamba, baada ya mama Diamond kusikia kuwa, mwanaye atarejea Bongo, Desemba 8, mwaka huu akiambatana na Zari alianza kuhaha kwa vile alishamtolea maneno makali akidai kuwa, mkwewe huyo alikuwa analeta uzungu kwenye familia yake.
“Unaambiwa ndugu wanapomuonesha mama Diamond picha za Zari akijiachia na Diamond na mtoto wao, Tiffah, anaamini kweli anaweza kuja Bongo jambo ambalo hataki kulisikia,” kilisema chanzo hicho.

MAMA DIAMOND KAMA MAGUFULI
Kufuatia hali hiyo ilitonywa kuwa, mama Diamond alifunguka kimipasho:
“Hata kama akija ataondoka kurudi kwao kama alivyokuja kwani ‘Hapa Kazi Tu’ kama ilivyo kauli mbiu ya Rais John Pombe Magufuli.”
Ili kupata mzani wa habari hiyo, mmoja wa vijumbe wetu alimtafuta mama Diamond kwa njia ya simu ambapo aliwaka mara tu baada ya kuulizwa ishu hiyo.
Katika majibu yake ya hasira, mama Diamond alisema haogopi lolote na yupo tayari kwa lolote.

MSIKIE MWENYEWE
“Siogopi chochote Zari kurudi hapa, kama atakuja, atakuwa amekuja kama alivyokuja mwanzoni na ataondoka hivyohivyo kama alivyoondoka awali.
“Sasa kwani nina hofu gani wakati niko nyumbani kwangu hapa? Watu watuache na waache unafiki wa kufuatilia mambo ya watu,” alisema mama D kisha akakata simu.

TUJIKUMBUSHE
Mapema baada ya Zari kujifungua mtoto wa Diamond, kuliibuka maneno ya mama mkwe huyo kutoelewana na mama Tiffah ambapo mara tu baada ya sherehe ya 40 ya mtoto huyo, Zari alitimka Bongo kwa maelezo kwamba hatarejea lakini sasa anaweza kuja kupambana tena na mama mkwe wake anayeonekana bado ana jambo moyoni.

Imeandikwa na Gladness Mallya, Mayasa Mariwata na Musa Mateja
GPL

Rais John Magufuli na Waziri Mkuu Majaliwa Wamuibukia Samia Suluhu Hassan Ofisini Kwake

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli (kushoto) akiagana na Makamu wake, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa (kulia) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Nov 30, 2015. Wa pili (kulia) ni Naibu Katibu wa Makamu wa Rais, Mohamed Khamis
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, (kushoto) akizungumza na Makamu wake, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, wakati Rais na Waziri Mkuu walipomtembelea Makamu Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Nov 30, 2015 kwa mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, (kushoto) akizungumza na Makamu wake, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, wakati Rais na Waziri Mkuu walipomtembelea Makamu Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Nov 30, 2015 kwa mazungumz

Zitto Kabwe Ayafungukia Makampuni Makubwa Tanzania Ambayo Yanakwepa Kodi....

By Zitto Kabwe
Kutoka Hotuba ya Waziri Mkuu 26.08.2011 – Makampuni yanayoogoza kwa kulipa kodi

Note: (Highlights)
Only one Mining company (the smallest i.e. - Resolute Mining), only one telecom company(Airtel Tanzania).
Household names like: 
MeTL, Bakhresa/Azam, IPP, VodaCom, Coca cola, Pepsi(SABCO), Serengeti Breweries, Barrick Gold, ACACIA, AngloGold Ashanti not seen. No oil marketing companies pia.
One can conclude that, TBL is the most profitable company in Tanzania, NMB is the most profitable Bank.
A public debate is needed. Hili ni tatizo kubwa.
Here under is the an extract from the Prime Minister speech; Sehemu ndogo ya hotuba ya Waziri mkuu.
Mheshimiwa Spika,
1. Nitumie nafasi hii kuwapongeza baadhi ya Walipakodi Wakubwa kwa Serikali na ambao wamefanya vizuri kati ya kipindi cha mwaka 2005 na 2011. Kwa kipindi hicho, Makampuni yaliyoongoza kwa kulipa kodi ni pamoja na:
  1. Tanzania Breweries Ltd. (Tshs 165.4b)
  2. National Microfinance Bank (Tshs 108.6b);
  3. Tanzania Cigarette Company (Shilingi Bilioni 92.1);
  4. National Bank of Commerce (Shilingi Bilioni 89.9);
  5. CRDB Bank Ltd. (Shilingi Bilioni 79.2);
  6. Tanzania Ports Authority (Tsh 76.8b);
  7. Tanzania Portland Cement (Tshs 73.4b);
  8. Airtel (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 63.6);
  9. Tanga Cement Company Ltd. (Tshs 43.6 b);
  10. Standard Chartered Bank Ltd. (Tshs 40.0b );
  11. Citibank (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 35.7);
  12. Resolute (T) Ltd. (Tshs 32.1b );
  13. Tanzania International Container Terminal Services (Shilingi Bilioni 25.9);
  14. Tanzania Distillers Ltd. (Tshs 13.4 b); na
  15. Group Five International (PTY) Ltd. (Tshs Bilioni 9.5).

2. Napenda kutoa rai kwa Makampuni yote Nchini kuiga mfano huu mzuri. Wito wangu kwa Makampuni, Wafanyabiashara Wakubwa kwa Wadogo na Wananchi wote ni kuongeza juhudi katika kufanya biashara zao ili zizalishe kwa wingi na kupata faida kubwa zaidi. Faida kubwa itachangia katika kuongeza Mapato ya Serikali kwa njia ya Kodi na hivyo kusaidia kukuza uchumi, kuongeza Pato la Taifa na la Mwananchi mmoja mmoja na kuondoa Umaskini. Niwadhihirishieni kwamba, Serikali inatambua umuhimu wao kwa maendeleo ya Nchi yetu na itahakikisha inaongeza juhudi zake za kuweka Mazingira Wezeshi kwa Makampuni hayo kufanya shughuli zao vizuri ili kuwezesha kulipa Kodi kwa mujibu wa Sheria.
Issues, issues, issues

Upotevu wa Makontena 349 Bandarini: Watu 12 Watiwa Mbaroni na Jeshi la Polisi

Kufuatia agizo la Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa la kuwataka watuhumiwa wa wizi wa makontena 329 katika bandari ya Dar es salaam kuchukuliwa hatua na Jeshi la Polisi, tayari Jeshi hilo limewashikilia watuhumiwa kumi na mbili wanaohusika na wizi huo.

Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam,  Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (CP) Diwani Athumani amesema kuwa, uchunguzi unaofanywa na wataalamu waliobobea katika makosa ya uhalifu wa kifedha umeweza kuwabaini watu kumi na mbili  ambao wamehusika na wizi huo.

“Kati ya watuhumiwa hao kumi na mbili, watano wanashikiliwa na Jeshi la Polisi na saba bado wapo katika upepelezi na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani,” alisema Kamanda Athumani.

Wanaoshikiliwa kutokana na tuhuma mbalimbali ni Kamishna wa Idara ya Forodha na Ushuru TRA Bw. Tiagi Masamaki, Meneja Kitengo cha Huduma za Ushuru  na Bi.  Habib Mponezia, Msimamizi Mkuu wa Kitengo cha Ushuru wa Forodha.

Watuhumiwa wengine ni pamoja na Bi. Eliaichi Mrema, Msimamizi Kitengo cha Mawasiliano ya Kompyuta  Bw. Haroun  Mpande na Mchambuzi Mwandamizi wa Masuala ya Biashara Bw. Hamis Omary.

Aidha Kamanda Athumani amewaomba wananchi wenye taarifa za ubadhilifu wa mali za Umma kuendelea kulisaidia Jeshi la Polisi katika kutekeleza majukumu yake.

Unajua Athari za Kuitana Sweet, Dear na Baby Kwa Watu Ambao Sio Wachumba ama Mke na Mume?

BABY ni neno la Kiingereza lenye maana ya mtoto, tena mara nyingi linatumika kwa mtoto mdogo. Pia lina maana nyingine ya mpenzi. Ni neno maarufu sana siku hizi; hata wazee kabisa, utasikia wanaitana baby!

Mbali na hilo, yapo maneno mengine kama sweet, dear, honey na mengine mengi. Maneno yote hayo ya Kiingereza, yana maana zaidi ya moja, lakini kubwa zaidi ni kumaanisha mpenzi, mpendwa (hutumika katika kuonesha mapenzi ya dhati kwa mwingine).

Leo nataka kukupa kitu kipya kabisa kichwani mwako. Unahitaji utulivu wa hali ya juu ili kujifunza hili. Ni maneno mazuri sana, ya kipekee lakini kwa upande mwingine ni hatari kwa sababu hukaribisha matatizo ambayo hayakutarajiwa na mtumiaji.

HUTUMIKA WAPI HASA?

“Dear, naomba uniamshe saa 12:00 asubuhi, kesho nina vikao vingi sana asubuhi,” inaweza kuwa kauli ya mume akimwambia mkewe, ambaye naye anamjibu: “Sawa sweet, usijali.”

Kwa hakika ndipo sehemu sahihi zaidi kutumika. Ni maneno yenye mshawasha mkubwa na huonesha penzi la dhati lililopo moyoni mwa mhusika kwenda kwa mpenzi wake.
Husisimua na kuongeza ladha ya mapenzi ya kweli. Kumuita mpenzi wako kwa majina ya kimapenzi 

huongeza zaidi upendo na msisimko wa moyo. Mwenzi hujiona wa kipekee na mapenzi huzidi kukua.
Kwa maana hiyo basi, ni sahihi zaidi kwa wapenzi kuitana majina niliyotaja hapo juu na mengine yanayofanana na hayo kwa lugha yoyote ile, ila iwe inatambulika vizuri na anayetamkiwa.

ATHARI SASA!

Kwa upande mwingine kuna athari za kutumia maneno hayo. Zama hizi, maneno hayo yanaonekana ya kawaida tu. Mtu yeyote anaweza kumuita yeyote mpenzi, honey, baby n.k. Hapo ndipo kwenye tatizo lenyewe.

Kwa ujumla wanawake ndiyo wanaongoza zaidi kuitana majina hayo. Wakati mwingine huenda mbali zaidi na kuwaita hata wanaume majina hayo ya kimapenzi. Si rahisi kuona athari zake kwa haraka na moja kwa moja, lakini zipo na wengi zimewasababishia matatizo. Ngoja tuone..

HUPUNGUZA THAMANI


Kama nilivyotangulia kusema awali, maneno 
niliyotaja hapo juu husisimua na kuongeza mapenzi. Kwa kuyatumia vinginevyo, basi kwa kiasi kikubwa huanza kukuathiri na kupunguza thamani ya neno lenyewe.

Kama unaweza kumwita mfanyakazi mwenzako dear, mtu wa jinsi sawa na wewe sweet ni wazi hata utakapomuita mpenzi wako au wewe kuitwa na yeye, halitakuwa na nguvu sana ya mapenzi kwa sababu ni neno ulilolizoea kila wakati.

HUKARIBISHA USALITI
Wakati mwingine unaweza kujikuta umeingia kwenye usaliti bila kutarajia. Veronica, mfanyakazi wa saluni moja ya kiume iliyopo Sinza, Dar alitoa ushuhuda ufuatao:
“Mimi naishi na mchumba wangu, tuna mtoto mmoja mwenye miaka mitatu. Nafanya kazi saluni. 

Tangu nimeanza hii kazi, nimejifunza kutumia maneno matamu ya kumfurahisha mteja na wakati mwingine kumfanya akupe tipu baada ya kumaliza kazi.

“Kuna kaka mmoja nilizoeana naye sana. Kama kawaida, huwa namkaribisha kwa kumuita dear au sweet. Wakati nikiendelea kumfanyia scrub, mazungumzo yetu hutawaliwa na dear, sweet, nikajikuta nimezidi kumzoea.

“Kwa sababu tulibadilishana namba, mara akaanza kuwa na mazoea ya kunitumia meseji, akija ananipa pesa, anaondoka. Mazoea yakazidi. Nikajikuta nimemzoea na kuna siku ambayo siwezi kuisahau kabisa.

“Ni siku niliyomsaliti mchumba wangu...mbaya zaidi na huyo jamaa naye ana mke wake. Niliumia sana, lakini naamini kama nisingekuwa na mazoea ya kumuita majina ya kimapenzi nadhani nisingeingia mtegoni. Moyo wangu unauma sana, najuta kumsaliti mpenzi wangu.”

Unaweza usione athari hii moja kwa moja, lakini ndugu zangu chukua jambo hili leo; wanaume wengi wakiitwa kwa majina ya kimapenzi husisimka sana – hujiona wenye bahati na mara hushawishika kuingia mapenzi.

Kama mwanamke hatakuwa makini atajikuta ametumbukia. Ya nini yote hayo, wakati unaweza kubadilisha mazoea hayo? 

ANGALIA TOFAUTI
Rafiki zangu, kati ya maneno niliyoyataja, kuna ambayo yanakubalika kutumiwa na wasio na uhusiano lakini wawe na undugu wa damu. Mathalani baba, mama, kaka, dada, shangazi nk.

Hakuna tatizo kumuita mtu mpendwa, lakini siyo baby, sweet, mpenzi na mengine yenye maana ya moja kwa moja ya kimapenzi. Umenipata? Akili za kuambiwa, changanya na zako kisha unazifanyia kazi! Chukua kinachokufaa!
Hadi wiki ijayo kwa mada nyingine. Wewe ni muhimu sana kwangu. 

TOA MAONI YAKO JE NI KWELI NIYASEMAYO?