Monday, January 25, 2016

Shilole Ametua kwa Kidume Mpya



Baada ya kumwagana na aliyekuwa mwandani wake, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, staa mwenye makeke wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ametua kwa kidume mpya ambaye ndiye mrithi wa Nuh ambapo wikienda iliyopita alijiachia naye ‘live’ wakiwa nchini Afrika Kusini ‘Sauz’.

Akizungumza na mwanahabari wetu kwa njia ya simu wikiendi iliyopita, Shilole alifunguka kwamba hataki tena ‘stresi’ kama alizokuwa akizipata kwa mpenzi wake huyo wa zamani hivyo sasa hivi anataka maisha ya furaha na jinsi gani ya kutumia akili yake ili kutengeneza fedha.
“Acha tu sasa hivi nipunguze machungu yangu maana sihitaji tena stresi, nimepumzisha akili yangu kwa mtu sahihi kabisa ambaye nafikiri yuko karibu yangu, mambo ya Nuh tupa kule,” alisema Shilole au Shishi.

Msanii huyo alifunguka kuwa maisha yake yamebadilika kabisa na hataki kuwa na kitu cha historia ambacho kilimuumiza na kumtesa kwani anataka maisha mapya kabisa ndiyo maana ameamua kutumbua majipu ambayo yalikuwa yakimsumbua.
Kwa upande wake Nuh alipotafutwa kujua mtazamo wake baada ya Shishi kumwanika mwanaume wake mpya, jamaa huyo hakuwa na la kusema zaidi ya kumtakia Shilole kila la heri.

Source GPL
ANDIKA MAONI YAKO HAPA CHINI

Author: