BAADA ya sintofahamu nyingi kuibuka katika mitandao ya
kijamii kuhusiana na picha za mpenzi wa msanii wa muziki wa kizazi
kipya, Nasib Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zari the boss Lady, kusambazwa
katika mitandao ya kijamii zikimuonyesha akibatizwa mtoni, mwenyewe
ameibuka na kuweka sawa sintofahamu hizo.
Akizungumza na mtangazaji, Millard Ayo kupitia kipindi cha
Top Twenty, Zari alikubali kuwa picha hizo ni kweli zinaonyesha tukio la
kweli la kubatizwa kwake lakini ilikuwa mwaka 2013 huku akishangazwa na
usambazaji wa picha hizo kwa mwaka huu wa 2016.
“Nikweli nilibatizwa na kuwa Mkristu ilikuwa mwaka 2013,
lakini sasa nina maisha mengine nimefuata dini ya mpenzi wangu, Diamond,
nashangaa kwa nini picha hizo za mwaka huo ziwe stori leo wakati ni
muda mrefu na sasa nina maisha yangu mengine,” alisisitiza Zari.
Aliongeza kwamba, licha ya kuwa na maisha yake mapya
anaendelea na mambo yake mengine kwa kuwa yupo na maisha mapya hivyo
anafuata dini ya mpenzi wake huyo ambaye ni maarufu na nyota katika
muziki wa Bongo Fleva nchini huku akiwa na idadi kubwa ya tuzo
zinazotokana na umahiri wa muziki wake.
Mtanzania