Friday, November 27, 2015

BEN POL: "COKE STUDIO NI HATUA KUBWA KWANGU KIMUZIKI"

Msanii wa muziki wa kizazi kpya nchini,Benald Paul ‘Ben Pol’ amesema ushiriki wake katika onesho la Coke Studio ni moja ya mafanikio katika safari yake ya muziki. 

Kauli hiyo aliitoa wiki hii kuhusu ushiriki wake kwenye onesho hilo linaloendeshwa na kampuni ya CocaCOla kwa kushirikisha wanamuziki wa Tanzania na nje ya nchi ambao wamekuwa wakifanya onesho la kuvutia. 

alisema anajivunia ushiriki wake katika maonesho hayo na amefanikiwa kujifunza mengi kuhusu fani ya muziki. 

Alisema anajisikia fahari kufanya kolabo kwa kushirikiana na wanamuziki wengi kutoka Kenya katika msimu huu wa Coke studio ambapo kwa hapa nchini onesho hilo linarushwa kila Jumamosi. 

Ben Pol alisema onesho ka Coke Studio linahamasisha vijana kujiamini na kuonesha vipaji vyao na aliwataka vijana wenzake kujiamini na kutokata taaa iwapo wataka kutimiza ndoto zao na kufanikiwa katika maisha.

Author:

0 comments: