Taarifa kutoka Mahakama kuu kanda ya Mwanza zinaarifu kuwa Familia ya Alphonce Mawazo na Chadema wameshinda kesi dhidi ya Jeshi la Polisi ya kuzuia mwenyekiti huyo wa Chadema Geita asiagwe jijini Mwanza baada ya kuuawa kinyama kwa kukatwa mapanga
Amri ya Jeshi la polisi kuwa Mawazo asiagwe Mwanza kwa kuwa kuna hofu ya kipindupindu imetupiliwa mbali na Mahakama hiyo.
Mahakama hiyo iliyoketi chini ya Jaji Lameck Mlacha imetoa ruhusa mwili wa Alphonce Mawazo kuagwa jijini Mwanza na imeagiza Jeshi la Polisi kutoa Ulinzi siku hiyo lakini Ulinzi huo usivuke mipaka.
Sehemu ya hukumu ya kesi hiyo inasema "Kazi ya Polisi ni kulinda raia na si kuzuia mazishi.."
0 comments: