Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amemshambulia kwa maneno mwanasiasa mkongwe wa Kenya ambaye pia ni kiongozi wa chama cha CORDS huku akimpiga marufuku kukanyaga ardhi ya nchi hiyo.
Akizungumza huko Marondela katika hafla iliyowahusisha wanajeshi walioshiriki katika vita mbalimbali, Mugabe alimtuhumu Raila kwa kutaka kumpindua kwenye nafasi yake kwa kuwapandikiza wapinzani nchini humo.
Hivi ndivyo alivyosema:
“Raila Odinga ni mwanasiasa muongo wa Kenya, mwanaume mnafiki ambaye yuko katika mkakati wa kuwapandikiza marafiki zake kuwa marais kwenye nchi zote za Afrika ili awe mwenyekiti mwenye nguvu kwenye Umoja wa Afrika (AU), siku moja watamuangusha kwenye sanduku la kura.
“Angalia alichokifanya Nigeria, Tanzania, Ivory Coast na anataka kufanya hivyo pia Uganda kwa kumtumia rafiki yake Kiiza Besigye ambaye leo anapewa sifa na ushupavu ambao anapata kutokana tu na amri za Raila barani Afrika.
“Hapa hatutamruhusu kuwageuza marafiki zake wa zamani Tendai Biti na Morgan kuniondoa mimi, hakuna kwa namna yoyote. Nitatawala kwa miaka 90 zaidi. Nimekiamuru kikosi maalum cha jeshi kuangusha ndege yoyote itakayokuwa imembeba huyo mwendawazimu Raila na kundi lake la mipango ya uchakachuaji wa kura dhidi ya marais wanaoendelea kutawala Afrika.
“Nimewaamuru walinzi wangu kuhakikisha wanakuwa makini kuhakikisha Raila hajipenyezi bila kubainika.
“Tutashindwaje kukosa usingizi kwa sababu tu ya Raila, yeye ni kitu gani? Tutamkamata na kumhasi kabla yeye na timu yake hawajamsaidia Morgan na Biti kunipindua kwenye Urais.”
Hii sio mara ya kwanza kwa Mugabe kushambulia Kenya kwa maneno, wiki chache zilizopita alidai kuwa wananchi wa Kenya ni wezi kutoka damuni na kwamba anadhani wanasomea shahada ya wizi. Alitahadharisha wananchi wake kutokubali kukaa karibu na wakenya kwa madai kuwa wanaweza kuwaambukiza wizi.
Mwezi Juni mwaka 2008, Raila Odinga aliwasilisha pendekezo lake mbele ya Umoja wa Afrika akitaka Umoja huo kumsimamisha uanachama Rais Mugabe hadi pale atakaporuhusu uchaguzi wa huru na haki nchini kwake.
| 10:52 PM
0 comments: