Mkurugenzi wa Freconic ideaz, Fred Ngimba (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu tamasha kubwa la burudani la Instagram Party litakalofanyika Jumamosi katika viwanja vya Escape One Mikocheni likiwa na kauli mbiu Bongo Throw Back. Kulia ni Meneja Mawasiliano, Krantz Mwantepele.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya Freconic Ideaz, imeandaa tamasha la burudani la ‘Instagram party’ litakalofanyika kesho kutwa kwenye Ukumbi wa Escape One Mikocheni jijini Dar es Salaam likiwa na lengo la kuwakumbusha wapenzi wa muziki, mavazi na misemo ya kizamani.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Freconic Ideaz, Fred Ngimba alisema pia tamasha hilo litahusisha watu wenye ushawishi mkubwa katika mitandao ya kijamii na wasanii mbalimbali wa muziki na filamu wanamichezo na wanasiasa na kuweza kufanikisha mashabiki wao kuweza kupiga nao picha katika red carpert.
Alisema wadau na marafiki mbalimbali wanaotumia mitandao ya kijamii watakutana siku hiyo kuweza kufahamiana na kubadilishana mawazo huku wakipata burudani mbalimbali.
“Kiingilio katika tamasha hili kitakuwa ni sh. 50,000 kwa viti maalumu na vile vya kawaida ni sh. 10,000, ambapo halitaishia hapa ila litaendelea katika Mikoa ya Mwanza, Morogoro, Tanga, Dodoma na Iringa,” alisema Ngimba.
Alitoa mwito kwa wadau wa muziki wa mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi kushuhudia burudani itakayotolewa siku hiyo kwani kuna maboresho makubwa yamefanyika katika kuongeza ubunifu
0 comments: