Monday, January 25, 2016

Arsenal yaongoza kwa mapato ya mechi duniani.

Arsenal wanatengeneza pesa nyingi kwenye siku za mechi kuliko klabu yoyote duniani – na imezipiku Chelsea kama klabu iliyoko juu kifedha jijini London kwa mara ya kwanza ndani ya miaka sita, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Deloitte.

Mapato ya ziada yalipatikana kwenye Uwanja wa Emirates wenye siti 61,000, uliofunguliwa mwaka 2006 na kuweza kuwafanya kuwa klabu kubwa barani Ulaya kutengeneza fedha nyingi kwa kila mechi ya nyumbani.

Arsenal inaongoza kwa mapato ya kila mechi duniani

Mwaka uliopita walitengeneza pauni milioni 101.84, wakiizidi Real Madrid, ambao waliingiza pauni milioni 100.1 kwenye mechi zao Bernabeu, na Barcelona, walipata jumla ya pauni milioni 90.17 kutoka Nou Camp.

Kwenye orodha hiyo inafuata Manchester United, wanatengeneza pauni milioni 87.96 kutoka Old Trafford huku Chelsea wakiwa wa sita pauni milioni 71.84 kutoka Stamford Bridge.
Uwanja wa Emirates ulizinduliwa mwaka 2006

Liverpool (57.85 pauni milioni), Manchester City (pauni 43.98m) na Tottenham (pauni 41.83m).

Author: