Baada ya zile tetesi za muda mrefu kuhusiana na kocha wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger kutokuwa na maelewano mazuri na mkewe Annie, stori kutoka mtandao wa mirror.co.uk
umethibitisha kutengana kwao, awali kulikuwa na uvumi wa wanandoa hao
kuachana kutokana na kutoonekana wakiwa katika picha ya pamoja toka
mwaka 2013
Stori kutoka mtandao wa mirror.co.uk
September 23 unaeleza wawili hao kutengana na kukubaliana kisheria
kugawana baadhi ya mali na fedha, kikubwa kinachotajwa kuharibu
mahusiano yao ni ubize wa Arsene Wenger katika klabu yake ya Arsenal. Wenger mwenye umri wa miaka 65 na mkewe Annie mwenye umri wa miaka 59 hawakuwa pamoja toka mwezi June mwaka huu.
Wenger na mkewe Annie
walifunga ndoa December 2010 baada ya kuwa katika mahusiano ya muda
mrefu na wamefanikiwa kumpata mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 18.
Nyaraka ya kisheria ya kifaransa “séparé du corps” haimaanishi kuwa Wenger na Annie wameachana kwa talaka ila haiwaruhusu kuishi pamoja.