Staa mkali wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu akiwa na aliyewahi kuwa bwana’ke (Linah), Nangari Kombo kitandani.
Staa wa Bongo Fleva almaarufu Ndege Mnana, Esterlina Sanga ‘Linah’, amedai kunasa ‘live’ tukio la mkali wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu akiwa kitandani na aliyewahi kuwa bwana’ke (Linah), Nangari Kombo ambaye alipata umaarufu mwaka 2010 alipoingia kwenye Uwanja wa Taifa, Dar na kumkumbatia Mchezaji wa Brazil, Ricardo Kaka kwenye mechi ya kirafiki kati ya timu hiyo na Taifa Stars.KUMBE PIA ALIKUWA MENEJA
Habari za kidaku zilidai kwamba, jamaa huyo ambaye amedumu na Linah kwa takriban miaka minne, pia ndiye alikuwa meneja wa msanii huyo ambaye alimsaidia mchakato wa kutengeneza video ya wimbo wake wa Ole Temba iliyofanyika nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’.
Ilifahamika kuwa Wema ambaye hivi karibuni alidai kufunga ndoa ‘hewa’ amekutwa na skendo hiyo ikiwa ni siku kadhaa tangu alipoonekana ‘veri klozi’ na yule staa wa Big Brother Africa ‘Hotshots’ 2014, raia wa Namibia, Luis Manana kwenye Shoo ya Instagram Party iliyofanyika katika Viwanja vya Posta, Kijitonyama, Dar, mwishoni mwa wiki iliyopita.
HAKUNA ALIYEJUA
Kama hiyo haitoshi, ilifahamika pia kwenye pati hiyo, pia Wema baadaye alionekana na Kombo lakini hakuna aliyejua kinachoendelea kwa kuwa alimtambulisha jamaa huyo wa Namibia kuwa ndiye mpenzi wake kwa sasa.
LINAH ACHARUKA
Ilidaiwa kwamba, baada ya Linah kuhakikishiwa kuwa Wema anatembea na Kombo alicharuka akitaka Wema amwachie mchumba’ke lakini alipoona maji yamefika shingoni aliamua kumwagana naye huku bado akimpenda.
“Unajua hii ishu siyo ya sasa hivi, ilianza kitambo sana, mwanzoni Linah alicharuka sana lakini alipoona yamemshinda akaachana na Kombo wakati bado alikuwa akimpenda sana,” kilisema chanzo chetu ambacho ni mtu wa karibu wa Linah.
TEAM WEMA
Ilisemekana kwamba, baadhi ya wafuasi wa Wema wanaojiita Team Wema ambao wanaijua ishu vizuri wamekuwa wakijibu mapigo kwa Linah huku wakimmwagia matusi ya nguoni kuwa huenda alishindwa ‘mambo f’lani’ ya chumbani ndiyo maana Kombo akahamia kwa Madam ambaye ‘eti ni mkali wa hizo kazi’.
LINAH ANASA PICHA ZA TUKIO
Habari za mjini ziliendelea kudai kwamba, katika kupata ushahidi, Linah alifanikiwa kunasa picha za Wema na Kombo wakiwa kitandani zilizomuonesha Wema akiwa na taulo pekee huku jamaa akiwa na ‘singilendi’ na boksa huku akionekana kutokwa na kijasho chembamba kwenye mashuka meupe hivyo kuwa na uhakika kuwa kuna kitu kinaendelea.
JE, NI PROJECT?
Tofauti na baadhi ya mastaa wengine ambao wamekuwa wakinaswa kimapenzi wakasingizia project ya kisanaa, ilidaiwa kwamba kwa Linah haamini hilo kwani hakukuwa na uhusiano wowote wa kisanaa kati ya Wema na Kombo.
HUYU HAPA NDEGE MNANA
Akizungumza na Risasi Jumamosi, juzi (Alhamisi) katika mahojiano maalum jijini Dar, juu ya ishu hiyo, Linah alisema kuwa alijua muda mrefu kwamba Wema anatembea na mpenzi wake huyo ambaye walikuwa wamefikia hatua ya uchumba.
“Kusema kweli nimeshaachana na Nangari (Kombo) na ninafahamu wazi kuwa anatoka na Wema Sepetu kwa sasa maana kuna picha kibao nimekuwa nikitumiwa zikionyesha wapo pamoja.“Mwenyewe kuna mahali nimekuwa nikiwakuta wako pamoja, jambo ambalo kwa sasa haliniumizi kichwa maana tumeshaachana na kila mtu ana mambo yake ila ninachoona kwa mwenzangu ameamua kuwa na Wema kama kuniumiza kichwa wakati kwa sasa naona ni kawaida tu.
“Kuna muda inafikia anakuwa kama anawatuma waje kuniambia maana kitu ambacho hata hakiniumi ila Wema naye namuona mtu wa ajabu sana kama yeye aliumizwa na ishu ya Kajala (Masanja) kumchukua CK wakati tayari alikuwa ameshaachana naye sasa kwangu mbona yeye kafanya hivyo.Staa wa Bongo Fleva almaarufu Ndege Mnana, Esterlina Sanga ‘Linah’ akiwa na aliyewahi kuwa bwanake Nangari Kombo.
“Ujue ingekuwa rahisi kwake kutoka na Nangari (Kombo) halafu mimi nisimuone wa ajabu kama angekuwa hajawahi kuniona naye lakini kwa sasa naye ameamua kufanya hivyo wakati anajua nilikuwa naye na mara kadhaa tulikuwa tukikutana tukiwa pamoja.“Hata hivyo, nawatakia mapenzi mema kwa kuwa sina mpango na Nangari (Kombo) tena ila ajue anachofanya naye ni ulimbukeni tu maana hata kama angeweza kuwa na Wema na asijioneshe kama hivyo kwa kuwa mimi siumizwi.
“Ila namshangaa Wema kumchukua mtu ambaye anajua alikuwa mtu wa rafiki yake ndiyo tatizo kwa kuwa yeye pia alishawahi kuwalaumu watu kwa ishu hiyo hadi leo hawazungumzi,” alifunguka Linah kwa uchungu kuonesha kukasirishwa na kitendo hicho.
WEMA VIPI?
Baada ya kuchukua maelezo ya Linah kinagaubaga, gazeti hili lilimsaka Wema kwa kila njia hadi kumfuata nyumbani juzi lakini liliambiwa kuwa amelala mchana wote na kila alipopigiwa simu haikuwa hewani hivyo jitihada za kusikia upande wake zinaendelea.
TUJIKUMBUSHE
Miezi kadhaa iliyopita, Linah na Kombo walitibuana na kutangaza kuvunja uchumba wao kwa kile kilichodaiwa kwamba kulikuwa na kundi la watu lililokuwa likiwachonganisha hivyo kila mmoja akachukua hamsini zake.
BAADA ya minong’ono ya muda mrefu, hatimaye staa wa Bongo Fleva, Estelina Sanga ‘Linah’ ameweka wazi kuwa anatoka kimapenzi na Nagari Kombo.
Linah alisema: “Ni kweli kwa sasa natoka na Kombo, ndiye mwanaume wangu, sina haja ya kuficha. Mimi na Amini imebaki stori tu, hata yeye ana mtu wake.”
0 comments: