Kwenye zile headlines za burudani leo 255 Producer wa The Industry Studios aliyetengeneza ngoma ya ‘GAME’ ya Navy Kenzo Feat.Vanessa Mdee amezungumzia beat ya ngoma hiyo kufananishwa na ngoma ya Girlie ‘O’ ya Patoranking feat.Tiwa Savage , amesema Watanzania wengi hawaamini wala hawapendi kuona wenzao wanafanya vizuri, lakini wanapaswa kujua wanafanya nini, anasema ana mazungumzo mazuri sana na Patoranking na kama kuna tatizo angemwambia.
Lameck Philipo au Bonge la nyau ametangaza a.k.a. nyingine ya jina lake kuwa ni Nyauloso, amesema wengine walikuwa hawalipendi wakisema jina ni baya lakini sasa hivi wanalipenda jina la ‘Nyauloso‘..anasema awali kuna msichana alimpa jina la ‘Big Cat’ na kulibadilisha kuwa ‘Bonge la Nyau’ na Nyauloso alipewa na x-girlfriend wake.
Joh Makini amezungumza na kusema walikua na maisha kabla ya kampeni lakini hawezi kusema kama walishindwa kufika bei na watu wa vyama kuhusu kufanya kampeni, anasema wanaepuka kupendelea vyama kwa kuwa wao ni kama wafanyabiashara wanasapoti sehemu yoyote na wanawaheshimu mashabiki wao.
0 comments: