Wednesday, September 16, 2015

Kisa Pombe; Johari Azima, Akombwa Kila Kitu

Kisa pombe! Mwigizaji wa kitambo Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ anadaiwa kupiga mitungi hadi akazima kisha kukombwa mkoba uliokuwa na kila kitu zikiwemo fedha taslimu Sh. 285,000/= na simu ya ‘tachi’ ya bei mbaya.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita kwa njia ya simu akiwa mkoani Tabora ambako Johari na baadhi ya mastaa wengine wapo kwa kazi maalum, mmoja wa wasanii hao alitonya kuwa tukio hilo lilijiri Alhamisi usiku, wakati wakiwa wanagida pombe, jambo lililozua taharuki kwake na wenzake.

Mtonyaji huyo alifunguka kuwa, wakiwa wanaendelea kunywa, Johari alifika wakati akazima ambapo walikuja watu waliojiita mashabiki wake, wakawa wanamvizia hivyo alipozinduka akaenda maliwatoni na kuacha mkoba wake, aliporudi ndipo akagundua kuwa mkoba wake haukuwepo, hali iliyomfanya aangue kilio cha uchungu.

Baada ya kupata ‘ubuyu’ huo, mwandishi wetu alimtafuta msanii rafiki wa damu na Johari (jina tunalo) ambapo aliombwa kumpa simu Johari ili kuzungumza naye ndipo Johari akakiri kukumbwa na masaibu hayo.

“Ni kweli tulikuwa tumekaa mahali ndipo nikalizwa mkoba wangu uliokuwa na vitu vyangu vyote,” alisema Johari.Kisa pombe! Mwigizaji wa kitambo Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ anadaiwa kupiga mitungi hadi akazima kisha kukombwa mkoba uliokuwa na kila kitu zikiwemo fedha taslimu Sh. 285,000/= na simu ya ‘tachi’ ya bei mbaya.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita kwa njia ya simu akiwa mkoani Tabora ambako Johari na baadhi ya mastaa wengine wapo kwa kazi maalum, mmoja wa wasanii hao alitonya kuwa tukio hilo lilijiri Alhamisi usiku, wakati wakiwa wanagida pombe, jambo lililozua taharuki kwake na wenzake.

Mtonyaji huyo alifunguka kuwa, wakiwa wanaendelea kunywa, Johari alifika wakati akazima ambapo walikuja watu waliojiita mashabiki wake, wakawa wanamvizia hivyo alipozinduka akaenda maliwatoni na kuacha mkoba wake, aliporudi ndipo akagundua kuwa mkoba wake haukuwepo, hali iliyomfanya aangue kilio cha uchungu.

Baada ya kupata ‘ubuyu’ huo, mwandishi wetu alimtafuta msanii rafiki wa damu na Johari (jina tunalo) ambapo aliombwa kumpa simu Johari ili kuzungumza naye ndipo Johari akakiri kukumbwa na masaibu hayo.

“Ni kweli tulikuwa tumekaa mahali ndipo nikalizwa mkoba wangu uliokuwa na vitu vyangu vyote,” alisema Johari.

Author:

0 comments: