Baada ya kuachana na mchumba wake miaka miwili iliyopita mwimbaji wa R&B Christina Millian alianza kuonekana sana na rapper Lil Wayne baada ya kujiunga na lebo ya msanii huyo, muda mfupi badaae wawili hao wakaingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na mpaka sasa wana zaidi ya mwaka mmoja pamoja.
Lakini leo headlines za wawili hawa ni tofauti kidogo… wapenzi hao wamethibitisha kuwa wameachana toka mwezi uliyopita lakni waliamua kukaa kimya kwanza na kuweka baadhi ya mambo yao sawa kabla kutangaza kwa watu kuwa uhusiano wao wa kimapenzi umeisha.
Msemaji wa karibu wa watu hao anasema sababu kubwa iliyopelekea kuachana kwao zinatokana na ratiba za wawili hao kubana sana.
>>>“Wanaachana sio kwamba wanapenda ila ratiba zao zinawabana sana, wanakosa muda wa kuonana na kuwa pamoja, Lil Wayne anafanya sana tour za wasanii wake na za kwake pia na pia anaifanyia kazi album ya Christina Millian… isitoshe hata Christina Millian ana mambo meng, vipindi vya TV, Talk Shows za kuandaa na vingine vingi, so wameona bora waachane lakini sio kwa sababu wamechokana ila ratiba za kazi haziwapi muda wa kuwa pamoja”. <<< Alisema msemaji wa karibu wa mastaa hao.
0 comments: