Diamond na Zari Hassan wamemuonesha mtoto wao Latiffah kwa mara ya kwanza Jumapili hii.Tiffah, mtoto wa Diamond Platnumz aliyezaa na mpenzi wake wa Uganda, Zari the Bosslady ni kama photocopy ya sura ya baba yake.
Tiffah
Mastaa hao wamesherehekea siku 40 tangu kuzaliwa kwa mtoto huyo maarufu kwa kualika marafiki na watu wa karibu kwenye hafla iliyofanyika kwenye makazi yao, wanayoyaita State House..
Mastaa mbalimbali wamehudhuria hafla hiyo ya kumtoa hadharani kwa mara ya kwanza mtoto huyo maarufu.
Akiongea kwenye kipindi cha EFM Uhondo kinachoendeshwa na mtangazaji wa zamani wa Clouds FM, Dina Marious, hivi karibuni Diamond alisema hana shaka kuwa Tiffah ni damu yake kukanusha tetesi zilizokuwa zimeenea kuwa huenda akawa si mwanae. Picha za mtoto huyo zimethibitisha ukweli huo.
Kaka wa Zari, Williams Bugeme akiwa na Tiffa
“Unajua mtoto kama si wako ni rahisi tu kujua. Na unajua mzazi anakuwa mtu wa kwanza kugundua kama mtoto si wako,” alisema Diamond. “Tena wazazi wetu wa Kiswahili wanakuaga sijui na machale gani akiona kama anasema ‘baba copy sio yako.’
“Yaani Latti ukimuona kabisa utasema ‘huyo Platnumz’.
Hizi ni comments za baadhi ya watu walioandika kwenye picha nyingine ya Tiffah aliyoiweka Zari kwenye ukurasa wake wa Facebook:
Vero James: Copy and paste of Diamond Platnumz Fans ‘ face. Congrats bro.
Haulah HK: This kid resembles Diamond Platnumz for real..awuchhii. eyes fr zari tho
0 comments: