Saturday, October 3, 2015

Ali Kiba na Hasheem wagongana kumuoa Jokate! Mkasa upo ha

mastaa katika category tofauti, Ali Saleh Kiba na Mtanzania anayecheza mpira wa kikapu nchini Marekani (NBA), Hasheem Thabit Manka, wanadaiwa kuchuana vikali kila mmoja akiwania kumuoa mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ huku mama mzazi wa mrembo huyo akitia ngumu, Risasi Jumamosi linaweza kuripoti.
TAARIFA ZA AWALI
Habari za awali, zilizovujishwa na mtoa taarifa wetu ambaye ni rafiki wa karibu na familia ya Jokate, juzi Jumatano zilieleza kwamba, kwa sasa kuna vita baridi kati ya Hasheem na Kiba kwa kila mmoja kutumia njia mbadala ili kuhakikisha anamuweka kibindoni mrembo huyo.
MPASUKO NDANI YA FAMILIA
“Lakini wakati hilo likiendelea, kuna taarifa kwamba kuna mpasuko kwenye familia ya Jojo (Kidoti). Inasemekana mama wa mrembo huyo anampa nafasi kubwa Hasheem.
“Lakini kwa upande wake, Jokate amekuwa akimnadi Kiba, jambo linalozua mpasuko mkubwa kwa familia hiyo,” kilinyetisha chanzo hicho.
Chanzo hicho kilishusha madai mazito kwamba, hivi karibuni baada ya Hasheem kusikia tetesi za kushamiri kwa penzi la Kiba na Jokate, alidaiwa kukwea pipa kutoka Marekani kisha akatua Bongo kimyakimya ambapo alifika nyumbani kwa akina Jokate, Oysterbay jijini Dar ili kujua mbivu na mbichi.
“Baada ya kuona hivyo, mama Kidoti aliitisha kikao cha dharura na kumtaka Jokate akubali kuolewa na Hasheem ili waishi maisha mazuri lakini bidada (Jokate) alilipinga vibaya na kushikilia alichokiita uhuru wa mapenzi na kwamba chaguo lake ni Kiba.
“Kiukweli hali mbaya sana kati ya Jokate na bimkubwa wake, mama anataka binti aolewe na Hasheem lakini Jokate anashikilia msimamo wa kuwa na Kiba,” kilinyetisha ‘kikulacho’ hicho.
Mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.
RISASI HADI KWA JOKATE
Ili kung’amua lipi ni tui na yapi ni maziwa juu ya madai hayo, mwanahabari wetu alisaga lami hadi ushuani, Oysterbay, Dar nyumbani kwa akina Jokate ambapo aliwakuta watumishi wawili ambao walimwambia mwandishi wetu kuwa Jokate na mama yake hawakuwepo, walitoka kwenda kwenye mihangaiko yao ya kila siku.
UDADISI WAANZA
Ili kupata chembechembe ya madai hayo, paparazi wetu alidodosa na kubaini kuwepo kwa sintofahamu kati ya Jokate na mama yake huku jina la Hasheem likitajwa kuwa alionekana maeneo hayo kama wiki mbili zilizopita.
JOKATE ‘BIZE’ MUDA WOTE
Baada ya kupata ‘ubuyu’ huo, mwanahabari wetu alimtafuta Jokate kupitia simu yake ya mkononi ambapo hakupokea licha ya kuita mfululizo.Hata alipotumiwa meseji kwa njia ya WhatsApp hakujibu licha ya kusomewa kila kitu.
Kwa upande wake, Kiba simu yake haikupatikana hewani huku Hasheem akielezwa amesharejea nchini Marekani.
TUMEFIKAJE HAPA?
Kabla ya kudaiwa kuwa mikononi mwa Mbongo-Fleva, Kiba, Jokate aliwahi kunasa kwenye penzi la mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akitokea kwa Hasheem ambaye ilidaiwa kwamba mrembo huyo alikufa kwake kiasi cha kutaka kujiua baada ya kuachana naye.

Author:

0 comments: