Uhuru Kenyatta |
Uamuzi wa Rais Kenyatta umekuja siku moja baada ya kutangaza ufisadi kama tishio la usalama wa kitaifa huku akiazimia kufanya mabadiliko makubwa kwenye ofisi ya Rais hivi karibuni.
Katika mabadiliko hayo, Kenyatta ameongeza pia idadi ya wizara kutoka 16 hadi 20 na kuongeza idara mpya chini ya wizara hiyo, kutoka idara 26 hadi 41 kwa kile alichoeleza kuwa ni kusaidia wizara kutekeleza majukumu yao bora zaidi.
Baadhi ya mawaziri walikuwa tayari wamekwisha jiondoa kwenye wizara zao kwa tuhuma za ufisadi huku wengine wakiwa na kesi za kujibu mahakamani.
Hivi karibuni, Waziri wa Ugatuzi, Anne Waiguru alikuwa wa mwisho kujiondoa kwenye wizara akiwa na kashfa zilizopata umaarufu zaidi kwa kipindi cha hivi karibuni za kununua kalamu moja kwa shilingi zaidi ya 200,000 za Tanzania.
Hata hivyo, Uhuru Kenyatta hakuwa na budi ya kuvunja baraza lake na kuunda upya kwa kuwa katiba ya nchi hiyo inataka idadi ya mawaziri isiwe chini ya 14. Baada ya Waiguru kujiuzulu nafasi ya uwaziri, baraza la mawaziri lilibaki na mawaziri 13 pekee.
0 comments: