Monday, November 30, 2015

KAULI YA LEMUTUZ KUHUSU KAMISHNA WA KODI TRA KUWA NA NYUMBA 73





Kazi za Magufuli ni kama hizi zinaonekana, watu mnalilia kuongoza tu mmekuwa Viongozi almost maisha yenu yote cha kuonyesha hamna maneno maneno mengi ya ulaghai na ujanja ujanja tulieni muonyeshwe maana ya Uongozi wa Taifa, tulieni muonyeshwe maana ya MABADILIKO huyu mjinga amejijengea nyumba zinazomzidi hata umri wake nyumba 73 hajafikia huo umri lakini tayari ana nyimba kushinda umri wake halafu unamlalamikia Magufuli unalalamika nini? .....mmewafamya.hawa wananchi wajinga for too long tumeimba wote MABADILIKO hapa yamekuja mnaanza kulia lia tena mnalia nini? Tulieni mlikuwa na nafasi ya kuongoza hakuna mlilofanya zaidi ya kila siku kutoa toa zawadi kwa wananchi zolizotokana na mapesa machafu tulikuwa tunajua ila hakuna marefu yasiyokuwa na ncha mwisho wa ujanja ujanja wenu umefika Magufuli hahahaha NAFWAZZZ ....kwa msiyoyajua ya huko ndani Magufuli ni noma sasa hivi sisi wote wananchi mbele yake tupo sawa kamkatalia mpaka Spika aliyetoka kuonana naye kabla uso kwa uso kabla ya uchaguzi wa Spika ikabidi Mama arudishe fomu mwenyewe na maneno mengi kwamba umri umepita nimeamua kupunzika kumbe Magufuli kakataa hata kukutana naye hahaha chezeiya Magufuli wewe...sasa wameshaanza kumlalamikia Magufuli ninasema hakuna aliyezaliwa kuwa Kiongozi tu yaani wewe ni lazima uwe waziri tu mazafantazz sio kweli waachieni na wengine bana hii ni zamu ya Magufuli na anaowataka tu na ikibidi wabakie watatu tu yaani Magufuli + Majawaliwa na Sefue kwani tunakimbilia wapi? ...maisha yenu yote mlikuwa mawaziri mmefanya nini zaidi ya kusafiri tu mambo sasa yamebadilika kubalini yaishe mlitubembeleza tumchague Magufuli Mabadiliko kumbe sasa inaonekana hata nyinyi wenyewe hamkujua mlichokuwa mnakiimba..Magufuli ndiye Rais anao washauri wake hahitaji washauri wa kujilazimisha Uongozi ni dhamana unapewa na wananchi sisi tumemuamini Magufuli kuwa Rais wewe tulia kwanza uamuzi wa anaotaka kufanya nao kazi ni wake ...MABADILIKO wananchi ndio haya hakuna aliye juu ya sheria tena kama.zamani hakuna rafiki au mshikaji wa rais kama zamani wote tupo sawa mbele ya rais mpya kama vepe subirini uchaguzi wa 2020!

Author:

0 comments: