Nkamia alisema "serikali kuu hutenga kiasi cha fedha kulingana na mahitaji na gharama halisi ya wakati husika.. Mwaka 2012 jumla ya shilingi Bilioni 43 zilitumika ambapo kati ya hizo Bilioni kumi na moja (11) zilitengwa na serikali na Bilioni 32 zilichangwa na mashirika, taasisi, makampuni na wadau mbalimbali walioombwa kuchagia kwa ajili ya kuadhimisha uzinduzi na kilele cha mbio za mwenge wa uhuru." Taarifa zinaonesha kuwa mwaka 2014 inakadiriwa jumla ya Shilingi Bilioni 120 zilitumika kama gharama ya kukimbiza Mwenge nchi nzima.
CALCULATION.
Bilioni 120 zinazotumika kukimbiza mwenge nchini (mwaka huu huenda zikaongezeka), zinatosha kufanya yafuatayo;
1. Kununua mashine 60 za MRI na CT Scan kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wenye kuhitaji vipimo hivyo. Ikumbukwe hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuna mashine moja tu ya MRI na moja ya CT Scan ambazo zote ni mbovu. Fedha za Mwenge zinaweza kununua mashine 60 za aina hiyo.
Rais Magufuli alijaribu kuhimiza ukarabati wa mashine hizo lakini zilifanya kazi kidogo tu kisha zikafa tena. Kwa sasa hakuna huduma za Vipimo vya MRI Hospitali ya Muhimbili, hadi imefikia hatua wagonjwa wametunga kirefu cha MRI kuwa ni;
-Magufuli -Rudi -Imeharibika tena.
2. Shilingi Bilioni 120 zinazotumika kukimbiza Mwenge zinatosha kulipia mikopo ya wanafunzi 61,624 wa vyuo vya Elimu ya Juu nchini. Hadi sasa takribani wanafunzi 40,000 walioko vyuoni hawajapata mikopo. Kumbe fedha za Mwenge zingeweza kuwalipia mikopo wanafunzi wote waliobaki na chenchi ikabaki (61624 -40000) x 1,960,000 = 4,238,304,000. Ikabaki chenchi ya Bilioni 4.2
3. Bilioni 120 za Mwenge zinatosha kujenga Zahanati 3,870 kwa gharama ya Mil.41 kila Zahanati. Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi mwaka huu Tanzania ina jumla ya Kata 3,802. Kwahiyo Bil.120 za Mwenge zinatosha kujenga Zahanati kila Kata nchini na chenchi ikabaki. (3870-3802) × 41,000,000 = 2,788,000,000. Ikabaki chenchi ya Bilioni 2.7
4. Bil 120 za Mwenge zinatosha kununua Boti 13 za kisasa za majini kama ile ya Bakharesa (Kilimanjaro 5). Ikumbukwe ukiondoa boti za Bakhresa, serikali haina usafiri wa kueleweka wa kwenda Zanzibar. Meli mbili za Mv. Spice Islanders na Mv.Scagget zilizama na kuua maelfu ya watanzania kutokana na uchakavu wa meli hizo. Kwahiyo Bil.120 za Mwenge zingeweza kununua meli mpya za kisasa kwa ajili ya usafiri wa Zanzibar na nchi jirani ktk bahari ya Hindi kama Msumbiji, Comoro na Kenya. Hii ingekua njia ya kuongeza pato la taifa kupitia sekta ya usafiri majini.
On other hand tungenunua Boti za kisasa tungeweza kupromote utalii wa fukwe (Beach Tourism). Nchi ya Mauritius inaingiza zaidi ya Shilingi Trilioni 10 kwa mwaka (nusu ya bajeti ya Tanzania) kupitia utalii wa fukwe tu. Mauritius hawana Mbuga za wanyama, hawana mlima mrefu kama Kilimanjaro, lakini wanapata Trilioni 10 kwa mwaka kupitia utalii wa fukwe, Tanzania tuna vivutio vya kila aina lakini tunaingiza Trilioni 1.7 tu kupitia sekta ya utalii.
Kwahiyo tukitumia fedha za Mwenge tunaweza kuboresha utalii wa fukwe na kuvutia watalii wengi zaidi na kupata mapato makubwa zaidi kutokana na sekta ya utalii.
5. Bil 120 za Mwenge zikikusanywa kwa miaka mitano (120 bil x 5 = 600 Bil) zinatosha kununua Ndege kubwa za kisasa zipatazo 10 angalau na sisi tukawa na Shirika letu la ndege. Kwa mujibu wa mtandao wa www.aircraftcompare.com bei ya ndege aina ya Boeing 737 yenye uwezo wa kubea abiria 240 ni USD 43 Million sawa na Shilingi za kitanzania Bil.80.
Kwahiyo Bil.600 za Mwenge (kwa miaka mitano) zinaweza kununua ndege kama 10 hivi angalau na sisi tukafufua Air Tanzania yetu tukaanza kushindana na Kenya Airways, Rwandan Air au Ethiopian Airways.
Kwa ujumla yako mambo mengi sn fedha za Mwenge zinaweza kufanya ikiwa zitatumiwa vzr. Hizi nilizotoa ni alternatives chache tu lakini kama viongozi wetu wakiwa makini wanaweza kufanya makubwa zaidi ya haya.
Written By Malisa GJ
0 comments: