Monday, November 30, 2015

Manispaa ya Ilala Jijini Dar, hupoteza takribani shilingi bilioni 2.9 kwa mwaka ambazo zinatakiwa kukusanywa kama kodi ya majengo.




Manispaa ya Ilala Jijini Dar, hupoteza takribani shilingi bilioni 2.9 kwa mwaka ambazo zinatakiwa kukusanywa kama kodi ya majengo. Hii inatokana na Serikali kushindwa kulipia majengo yake na malumbano ya ndani ya Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo. Meneja wa Kodi ya Majengo wa Manispaa hiyo, Stella Mgumia, amekiri kutofuatwa kwa taratibu zote za msingi katika zoezi la ukusanyaji wa kodi hiyo. Amesema katika mwaka unaokuja wanatarajia kuwahamasisha madiwani ili waweze kuwahamasisha wananchi kulipa kodi ya majengo, ikiwani utekelezaji wa mipango ya halmashauri hiyo. Moja ya changamoto kubwa inayotajwa kuchangia tatizo hilo ni pamoja na baadhi ya wamiliki wa majengo hususani kuwepo kwa wazee wasiotaka kulipa kodi licha ya kumiliki majengo ya kibiashara. Imeelezwa kwamba wazee wanaopaswa kutolipia kodi ni wale wanaoishi kwenye majengo ya wasiyoyatumia kibiashara.

Kutoka jamii forum Tanzania

Author:

0 comments: