Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu na watendaji wengine wa taasisi hiyo na kuagiza vyombo mbalimbali kufanya uchunguzi wa matumizi ya fedha katika mamlaka hiyo.
Pia, ameiagiza Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Ushirikiano wa Kimataifa na Kikanda kuwarejesha nyumbani mabalozi wawili ambao mikataba yao imekwisha.
Mwaimu anaingia kwenye orodha ndefu wa wakuu wa mashirika na taasisi za
Serikali waliosimamishwa au utezi wao kutenguliwa, kutokana na sababu
mbalimbali tangu Rais Magufuli aingie madarakani mwaka jana.
Baadhi ya waliotemwa ni aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward Hoseah, Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Bandari (TPA), Awadhi Massawe, Mwenyekiti wa Bodi ya TPA, Profesa Joseph Msambichaka, Kamishna Mkuu TRA, Rished Bade, Kaimu Mkurugenzi wa Muhimbili, Dk Hussein Kidanto, Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile na Kamishna wa Uhamiaji anayeshughulikia Utawala na Fedha, Piniel Mgonja see more http://www.mwananchi.co.tz/…/…/3049214/-/w70bc5/-/index.html