Friday, November 27, 2015

Waziri Mkuu akutana na hasara ya Bilioni 80 Bandarini


Huko tunakokwenda naona minyukano live.......mie simoooo kazi yangu nafikisha habari tujadiliane.... . . "Siku moja tu ya ziara Waziri Mkuu amekutana na hasara ya Bilioni 80 Bandarini. Hizi ni fedha ambazo zinatosha kuwapa mkopo wa biashara vijana 40,000 wa Kitanzania kila mmoja akapata milioni 2. Pia zinaweza kujenga mabunge mawili yenye hadhi sawa na bunge la Dodoma na zikabaki Bilioni 10 (Bil 35 x 2). Ni fedha ambazo ukiziweka katika noti za elfu kumikumi unaweza kuzitandaza umbali wa kilomita 960 (Bil 80 ÷10,000/= × 12 ÷100,000). Kilomita 960 ni umbali wa kutoka Tunduma hadi Dar. Yani ukatandaza elfu 10 kutoka Tunduma, Mbeya, Makambako, Iringa, Mikumi, Moro hadi Dar bila kuacha hata sentimita moja njiani. Halafu tunaambiwa hii wizara ilikua na Waziri. Tena maWaziri wawili walioitwa maJembe. Mwakyembe na Sitta kwa nyakati tofauti. What a shame?? Majembe wezi? MaJembe ya kupiga dili na watu wa TRA? MaJembe yamekaa wizarani miaka mitano yakashindwa kuona Bil.80 zikipotea, Majaliwa amekaa wiki moja ameweza kuona.! Mwakyembe, Sitta, Saada Mkuya ni wezi kama wezi wengine. Halafu eti walitaka Mwakyembe apewe Uwaziri Mkuu na Sitta Uspika??. Hahahaah People are not serious.!. Nadhani zawadi inayowafaa Mwakyembe na Sitta kwa sasa ni kuvuliwa Ubunge na kushtakiwa kwa uzembe na matumizi mabaya ya ofisi. Huwezi kuwa Waziri halafu zinapotea Bil.80 kila baada ya miezi michache afu hajaona. Seriously?? #Magufuli kamata Mwakyembe, Saada Mkuya, ongeza na Sitta, then changanya na yule Mkurugenzi wa TRA weka ndani wote.

Author:

0 comments: