Vyama vinavyounda Ukawa vimemshukia Rais John Magufuli, kuwa ndiye
anayekwamisha kutangazwa kwa rais aliyechaguliwa Zanzibar Oktoba 25,
mwaka jana.
Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alisema hayo jana wakati akitoa taarifa ya kikao cha Ukawa kilichofanyika juzi.
“Dk Magufuli akiamua wakati wowote matokeo ya Zanzibar
yatangazwe yatatangazwa. Serikali ya CCM imekuwa ikiwapangia Wazanzibari nani awe rais wao tangu kifo cha Karume (Abeid Aman) mwaka 1972,” alisema.

Mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe alisema Rais Magufuli ndiye anayepaswa
kulaumiwa kama amani itakosekana Zanzibar. “Ukawa tumeamua kusubiri
uamuzi wa Baraza Kuu la CUF ambalo linakutana kesho (leo) Dar es Salaam
na baada ya kutoa tamko lao, wabunge wa upinzani wataunga mkono.”
“Magufuli anayevaa magwanda amesahau kuwa yeye ndiye mkuu wa majeshi ambayo yanazunguka mitaa ya Zanzibar. Majeshi yanayowatishia Wazanzibari yako chini yake,” alisema Mbowe huku akisisitiza kuwa Dk Magufuli hawezi kukwepa kupatikana kwa haki Zanzibar http://www.mwananchi.co.tz/…/…/3049274/-/dkg7et/-/index.html

Vyama
vinavyounda Ukawa vimemshukia Rais John Magufuli, kuwa ndiye
anayekwamisha kutangazwa kwa rais aliyechaguliwa Zanzibar Oktoba 25,
mwaka jana.
mwananchi.co.tz