TETESI ZA SOKA ULAYA - JUMANNE 26.01.2016
Meneja wa Manchester United Louis van Gaal, alikuwa tayari kujiuzulu
siku ya Jumamosi baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Southampton, lakini
akabembelezwa asifanye hivyo na makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Ed
Woodward (Sun), Van Gaal ambaye amekwenda Uholanzi kwenye sherehe ya
kuadhimisha kuzaliwa kwa binti yake, ataendelea na mazungumzo na Ed
Woodward siku ya Jumanne atakaporejea (Guardian), Ed Woodward
amezungumza na wachezaji kadhaa, pamoja
na maafisa wengine wa ngazi ya juu Old Trafford kuhusu Van Gaal (Sky
Sports), hata hivyo Ed Woodward yuko tayari kwenda kinyume na mtazamo wa
mashabiki wengi na kuamua kumuacha Van Gaal aendelee kusalia Old
Trafford (Mirror), mwandishi wa habari Miguel Delaney amesema Manchester
United wanafahamu kuwa Jose Mourinho anataka kumrithi Van Gaal na kuwa
mazungumzo kati ya wawakilishi wake na United yamekuwa yakiendelea kwa
muda (BBC Radio 5 live), mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale, 26,
ameogopa kuhamia Manchester United kwa pauni milioni 100 kutokana na
hali ya mashaka iliyopo sasa kuhusiana na Van Gaal (Independent), winga
wa Tottenham Andros Townsend, 24, anakaribia kukamilisha uhamisho wake
kwenda Newcastle, baada ya timu hizo mbili kukubaliana ada ya uhamisho
(Guardian), Totteham wana wasiwasi kuwa huenda beki Jan Vertonghen, 28,
aliumia zaidi goti lake na huenda asicheze msimu wote uliosalia (Sun),
Newcastle watapanda dau jingine kutaka kumsajili Alexandre Lacazette,
24, kutoka Lyon, baada ya mchezaji huyo kusema hataki kwenda Newcastle
(Telegraph), Liverpool wamegonga mwamba katika dau lao la pauni milioni
28 kutaka kumsajili mshambuliaji wa Shakhtar Donetsk, Alex Teixeira,
ambaye amepachika mabao 22 katika mechi 15 msimu huu (Mail), West Brom
wanataka kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Mario Balotelli, 25,
anayechezea AC Milan kwa mkopo (Express & Star), matumaini ya
Newcastle kumsajili Loic Remy, 28, kutoka Chelsea yatategemea na
kukamilika kwa usajili wa Alexandre Pato kutoka Corinthians kwenda
darajani (Chronicle), Sunderland kwa mara nyingine tena wamehusishwa na
mshamuliaji kutoka Ivory Coast, Seydou Doumbia, 28, anayecheza Roma na
ambaye inadaiwa amekataa mkataba wa fedha nyingi kwenda China
(Sunderland Echo), West Ham wamekubaliana na mshambuliaji kutoka Nigeria
Emmanuel Emenike, 28, lakini bado hawajaafikiana na klabu yake
Fernabahce, na Al Ain ya Imarati anapocheza kwa mkopo (Evening
Standard), Watford wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa
Fiorentina Mario Suarez, 28 (Watford Observer). Hayo ni baadhi ya
yaliyoandikwa kwenye baadhi ya magazeti ya Ulaya. Zimealia siku sita
kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.
Cheers!!